Header Ads Widget

NEC YAPOKEA RUFAA 557 ZA UBUNGE NA UDIWANI, YAANZA KUSIKILIZAMwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistlocles Kaijage

Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC imetangaza kuanza kusikiliza rufaa zilizokatwa na wagombea wa ngazi za ubunge na Udiwani kutoka majimboni ambapo hadi Sasa tayari imepokea rufaa 557 ambazo inaanza kuzishughulikia mara Moja kuanzia leo.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semiostcles Kaijage ambapo amefafanua kuwa hatua hiyo inajiri baada ya kukamilisha mchakato wa Uteuzi wa majina ya wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kwa nafasi ya Urais hii leo.

"Leo tumeanza kuzisikiliza Rufaa zilizowasilishwa na wagombea waliokata kutoka majimbo mara baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya awali, baada ya kusikiliza tutatoa maamuzi kulingana na sheria na taratibu zilizopo"

Wakati huo huo tume imetoa wito kwa makundi mbalimbali kuendelea kuheshimu sheria za uchaguzi zilizowekwa Ili kuhakikisha kila raia mwenye haki ya kupiga kura wanatimiza wajibu wao kikatiba.