Header Ads Widget

CCM YAFAFANUA MATIBABU YA WASANII WALIOPATA AJALI

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole.

Chama cha Mapinduzi kimesema kuwa kinafuatilia kwa ukaribu na kuhakikisha wasanii watatu ambao ni Luludiva, Belle9 na Bonge la Nyau ambao wamepata ajali hii leo wakati wakitokea mkoani Iringa wanapata matibabu haraka.

Taarifa hiyo ya CCM imetolewa hii leo Septemba 7, 2020, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Hamphrey Polepole kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Chama Cha Mapinduzi tumepokea kwa mshtuko taarifa za ajali mbaya ya gari iliyowahusisha wasanii Belle9, Luludiva na Bonge la Nyau, tunafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wanapata huduma ya matibabu haraka na tunamwomba Mungu awape wepesi na kupona haraka", imeeleza taarifa ya Polepole.

Wasanii hao wamepata ajali majira ya Alfajiri hii leo, katika eneo la Chalinze wakati wakitokea Iringa, huku chanzo wakieleza kuwa ni Lori kuwachomekea kwa mbele, ndipo dereva wao akalitumbukiza gari kwenye korongo ili wasigongane uso kwa uso.