Header Ads Widget

KITANDULA AZINDUA KAMPENI MKINGA, SHEKIFU, KIGODA, MEJA KUNTA WAMUOMBEA KURA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula (kulia) akipokea ilani ya CCM kutoka kwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu wakati alipozindua kampeni za ubunge jimboni humo katika  eneo la Duga Maforoni wilayani Mkinga

Na Mwandishi Wetu, Tanga
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dastan Kitandula amezindua rasmi kampeni zake leo Septemba 6, 2020, huku akiwaomba wananchi kumchagua tena kuwatumikia kwa kipindi cha miaka mitano ili aweze kumalizia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Kero kubwa ambazo zimekuwa zikilikabili jimbo hilo ni maji na barabara ambapo alihaidi kuzipatia ufumbuzi wa kina wakati atakapopewa ridhaa ya kuwatumikia wananchi hao.

Uzinduzi wa kampeni hizo ulifanyia katika Kijiji cha Duga Maforoni wilayani humo ambapo ilizinduliwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu.

Kitandula amesema kuwa alipopata ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000, jimbo hilo lilikuwa nyuma kimaendeleo lakini hadi sasa asilimia 90 ya vijiji vimeunganishiwa na umeme wa REA na miradi ya maji, barabara na elimu imetekelezwa kwa asilimia kubwa.

Amesema hivi sasa baadhi ya vijiji ambavyo vilikuwa vikikabiliwa na uhaba wa maji wananchi wanapata maji safi na salama na kutolea mfano wa kijiji cha Mapatano.

Mgombea huyo alisema Kijiji cha Doda wakazi wake wame unganishiwa maji kupitia mradi wa mabwawa uliogharimu Sh Bilioni 1.4 wakati kata ya Duga Sigaya wananchi wanapata maji kutokana na mradi wa Sh Bilioni1.2 .

Kitandula ambaye anatetea kiti hicho alisema iwapo atachaguliwa tena kushika ubunge wa jimbo hilo atahakikisha anatia msukumo Serikalini ili mradi mkubwa wa kutoa maji Mabayani Jijini Tanga na kuyafikisha hadi mpaka wa Tanzania na Kenya wa Horohoro unatekelezwa.

Akizungumzia suala la umeme, Kitandula alisema wilaya ya Mkinga ina jumla ya vijiji 85 ambapo 65 vimesha unganishiwa nishati hiyo huku vijiji 20 vilivyobaki vikiwa vipo katika hatua za mwisho za mchakato wa kupatiwa umeme kupitia REA.

“Mkinichagua kushika nafasi hii nitahakikisha umeme sasa unapelekwa ngazi ya vitongoji vilivyopo katika vijiji vyote 85 na mtandao wa barabara utaongezeka zaidi”alisema Kitandula.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Duga Maforoni wilayani Mkinga wakati wa uzinduzi wa kampeni zake 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Mkinga, kulia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Dastan Kitandula
Dastan Kitandula akiwa ameshika ilani ya CCM mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu wakati wa uzinduzi wa kampeni wa Jimbo hilo
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Tanga, Dkt Aisha Kigoda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hizo
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Husna Sekiboko akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mwantumu Zodo akisisiitiza jambo wakati wa uzinduzi huo
MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) kupitia kundi la UWT Taifa Catherine Kitandula akizungumza wakati wa uzinduzi huo
SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
Sehemu ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Meja Kunta akitumbuiza wakati wa kampeni hizo