Header Ads Widget

ACT- WAZALENDO WATANGAZA NEEMA SHINYANGA MJINI, KUONGEZA MZUNGUKO WA FEDHA


Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya ACT - Wazalendo, Godwin Makomba akimwaga Sera zake kwa wanachi ili wamchague.

Na Marco Maduhu - Shinyanga
Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Godwin Makomba kupitia chama cha (ACT-Wazalendo), ameahidi endapo akishinda kuwa mbunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu, atafufua bandari kavu ya mjini humo ili kuongeza mzunguko wa fedha na kutoa ajira kwa vijana.

Alisema Shinyanga mjini inazidiwa na wilaya ya Kahama kwa mzunguko wa kifedha, sababu ya kuwa na viongozi wasio na maono ya kimaendeleo, hivyo yeye akiwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha ana jenga miundombinu ya mzunguko wa kifedha, ikiwamo na kufufua Bandari kavu pamoja na kiwanda cha Nyama.

Makomba alibainisha hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Chama hicho katika jimbo la Shinyanga mjini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Soko kuu la mjini Shinyanga, na kuhudhuliwa na viongozi wa kitaifa wa chama hicho, pamoja na wagombea Nane wa udiwani.

Alisema Jimbo la Shinyanga mjini miaka yote limekuwa likiongozwa na wabunge kutoka chama cha mapinduzi CCM, ambao hawana maoni ya kimaendeleo, bali wakipata ubunge wanapotea jimboni, lakini kwasasa yeye ndiye mkombozi wa wana Shinyanga hivyo ameomba wamchangue ili awaletee maendeleo na mzunguko wa fedha kwa kufufua bandari kavu.

“Naombeni wana- Shinyanga siku ya Oktoba 28 mnipigie kura ili niwe mbunge wenu na niwaletee maendeleo, ambapo nitafufua Bandari kavu ambayo ipo hapa mjini Shinyanga, na kuleta mzunguko wa kifedha ambapo kutakuwa na muingiliano wa biashara mbalimbali,”alisema Makomba.

“Pia nitakifufua kiwanda cha Nyama ambacho kimekufa na kukuza ajira kwa vijana, nitajenga na Soko kuu ambalo kila mwaka wa uchaguzi limekuwa kama sehemu ya kuombea kura, sasa mimi nitalijenga, ila msifanye makosa tu siku ya Oktoba 28, mnipigie kura ili nishinde na kuyatekeleza haya kwa kuyasemea Bungeni,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Makomba alitoa ahadi ya kuongeza ujenzi wa madarasa kwa shule za manispaa ya Shinyanga, ili kuondoa mrundikano wa wanafunzi madarasani, na kubaki wakisoma wanafunzi 45 kwa kila darasa, na siyo 80, 100 hadi 120, na kuwafanya kushindwa kuelewa masomo na kuambulia kupata Zero.

Naye mwenyekiti wa ngome ya wanawake taifa kutoka Chama cha ACT- Wazalendo Mkiwa Kimwanga, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni za chama hicho Jimbo la Shinyanga mjini, aliwataka akina mama kuacha kurubunika na Kanga, bali wasifanye makosa kwenye uchaguzi wa kuchague viongozi makini watakaowaletea maendeleo.

Pia aliwataka siku ya kupiga kura wakachague wagombea wote wa ACT-Wazalendo, akiwamo mgombea urais wa chama hicho Benard Membe, ili wawaletee maendeleo pamoja na kutoa ajira elfu 10 ndani ya miaka yao mitano ya utawala.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mwenyekiti wa ngome ya wanawake Taifa ACT-Wazalendo Mkiwa Kimwanga, (kulia), akimkabidhi Ilani ya Chama hicho Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Godwin Makomba.

Mwenyekiti wa ngome ya wanawake Taifa ACT-Wazalendo Mkiwa Kimwanga,akimwaga sera kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwenye ufunguzi wa kampeni ya chama hicho Jimbo la Shinyanga mjini.

Katibu wa ACT- Wazalendo Mkoa wa Shinyanga Merykyoli Tafuta, akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho Jimbo la Shinyanga mjini.

Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Shinyanga mjini Twaha Makani. akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho Jimbo la Shinyanga mjini.

Katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha ACT- Wazalendo Omari Gindu, akizungumza kwenye uzinduzi wa chama hicho Jimbo la Shinyanga mjini.

Baadhi ya viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni jimbo la Shinyanga mjini.

Baadhi ya viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni jimbo la Shinyanga mjini.

Baadhi ya wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Shinyanga mjini.

Baadhi ya wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Shinyanga mjini.

Baadhi ya wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Shinyanga mjini.

Baadhi ya wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha ACT-Wazalendo Jimbo la Shinyanga mjini.