Header Ads Widget

SIMBA YAISHINDILIA VITAL' O 6-0 TAMASHA LA SIMBA DAY


Mshambuliaji wa Simba, Christopher Mugalu akipongezwa na Clotous Chama baada ya kuifungia timu yake bao la tano.

WEKUNDU wa Msimbazi wamehitimisha kilele cha tamasha la CHAMPIONS WEEK: Another Level katika SIMBA DAY kwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya wageni wao, Vital'O Club ya Burundi.

Mabao ya Simba yamefungwa na Bernard Morrison, John Bocco, Ibrahim Ajibu, Clotous Chama, Christopher Mugalu na Charles Ilanfya.

 Bernard Morrison akifurahia baada ya kuifungia timu hiyo bao la kwanza

Nahodha wa Simba, John Bocco baada ya kufunga bao la pili kwa timu yake katika mchezo huo

Picha kwa hisani ya Simba SC Tanzania