Header Ads Widget

KAYA 100 KOLOMIJE, MONDO WILAYANI MISUNGWI ZABORESHEWA MAKAZI



Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza na wananchi wa Kata ya Koromije kabla ya uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kuboresha Makazi yenye kauli mbiu isemayo “Piga kazi boresha Makazi” iliyofanyika Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza. 

Na Wizara ya Afya, Misungwi
Zaidi ya Kaya 100 katika Kata za Koromije na Mondo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza zimeondokana na makazi Duni na kuboresha makazi yake ikiwa ni sehemu ya kuboresha maisha na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi.

Hayo yamebainika Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya uboreshaji makazi uliofanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. John Jingu.

Akizungumza katika Uzinduzi huo, Katibu Mkuu Dkt. Jingu amesema baada ya kutembelea makazi ya watu walioboresha makazi na kushuhudia uboreshaji wa makazi hayo ambapo wananchi kwa asilimia kubwa wameweza kuchukua hatua ya kuboresha makazi yao.

Aidha amewataka watanzania katika maeneo mengine nchini kuiga wanavikundi wa Kata ya Koromije kutumia mfano huo kuleta mabadiliko katika maisha yao ikiwa ni namna bora zaidi ya kuweza kujikwamua kutoka katika hali duni.

“Katika maeneo yote tumeshuhudia dhana ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na hali hii imeimarisha familia Ustawi na maendeleo na katika kuratibu mwongozo wa makazi bora hapa maafisa Maendeleo ya Jamii wafanye kazi kuhamasisha jamii, kuboresha makazi yao”

Dkt. Jingu amesisitiza kuwa mchango wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali ni muhimu sana katika Kampeni hiyo kwa kushirikiana na Serikali kuleta maendeleo ya wananchi hivyo Asasi za kiraia zione umuhimu wa kuunga Mkono juhudi za Serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda amewahimiza viongozi katika ngazi mbalimbali kuhamasisha Kampeni ya ujenzi wa makazi bora ili kuchochea maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Naye mmoja ya wafaidika wa Kampeni ya Kuboresha Makazi Bi Joyce Lupemba amesema mwanzo walikua wakiishi katika mazingira duni wakilala pamoja mifugo pamoja ila baada ya kuboresha makazi wamekuwa wakiishi na kulala sehemu salama.

“Tulikuwa tukisumbuliwa na wadudu wakiwemo chawa na kunguni, lakini kwa sasa wamejenga nyumba zinazowezesha kuishi kwa raha lakini pia nyumba bora zinasaidia katika malezi ya watoto”alisisitiza

“Mimi na familia tulikuwa tukilala katika nyumba ya tembe iliyoezekwa kwa nyasi huku nyumba hiyo hiyo ikitumika kama zizi la Mifugo, jambo lililochagia maambukizi ya magonjwa mbalimbali hasa kwa watoto” alisema

Aidha Shuhuda mwingine Bw. Tano Kakunga ameiomba Serikali kuboresha utoaji wa mikopo kwa vikundi ili waweze kuendelea kuboresha makazi zaidi hasa kwa kuwa na maji na umeme wa uhakika.

“Tulikuwa tukiishi katika nyumba za nyasi na udongo ilitulazimu kutolala nyakati za usiku mvua inaponyesha tukihofia nyumba zetu kubomoka na kujaa maji ndani” alibainisha

Kampeni ya kuboresha makazi inaenda na Kauli Mbiu Piga Kazi, Boresha Makazi, inayoenda sambamba na kauli mbiu ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi tu hivyo kauli ikiakisi mwelekeo wa kubadilisha hali duni na kuwa na maisha mazuri.
 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (mwenye miwani) akipiga ngozi ya ng’ombe mara baada ya kuwasili katika Kata ya Koromije Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza katika uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kuboresha Makazi yenye kauli mbiu isemayo “Piga kazi boresha Makazi”

 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimniana na Bi. Joyce Lupemba mkazi wa Kata ya Koromije alipomtembelea nyumbani kwake kushuhudia alivyoboresha makazi kutoka nyumba ya nyasi mpoaka ya tofali na bati katika uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kuboresha Makazi Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisoma kitabu cha muongozo wa uboreshaji wa Makazi wakati alipotembelea banda la Idara ya Maendeleo ya Jamii wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kuboresha Makazi yenye kauli mbiu isemayo “Piga kazi boresha Makazi” iliyofanhyika Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.
 
 Baadhi ya wakazi wa Kata ya koromije Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakfuatilia hotuba Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya kuboresha Makazi.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW