Header Ads Widget

ALIKIBA, DK. MWAKYEMBE WAINOGESHA AZAM FESTIVAL, AZAM IKIICHAPA NAMUNGO 2-1


Mfalme wa muziki nchini, Alikiba akitoa burudani kwa mashabiki wa soka na wapenzi wa timu ya Azam FC walioujaza Uwanja wa Azam Complex katika kilele cha Tamasha la Azam FC Festival. Picha zote kwa hisani ya Azam Football Club

Na Shinyanga Press Club Blog


Pichani ni Waziri Mwakyembe akiwa na Mkurugenzi wa Makampuni ya Bakhresa Group, Abubakar Bakhresa.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Harrison Mwakyembe, ndiye mgeni rasmi wa Tamasha la Azam FC Festival, akimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambaye amepata udhuru.

Leo Klabu ya Azam imeadhimisha kilele cha tamasha lao la 'AZAM FESTIVAL' katika uwanja wa Azam Comple, Chamazi jijini Dar es Salaam lililokuwa maalum kwa ajili ya kutambulisha kikosi na benchi la ufundi la timu hiyo kwa msimu mpya wa mwaka 2020/2021 na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC ya Lindi ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Sehemu ya waliojitokeza katika tamasha hilo kutoa burudani ni Msanii wa Kizazi kipya nchini, Alikiba ambaye aliwapagawisha mashabiki na wapenzi wa soka waliofurika uwanjani hapo.

Tamasha hilo linafanyika ikiwa ni siku moja baada ya tamasha la SIMBA DAY lililoadhimishwa jana kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, ambapo Msanii Diamond Platinumz alitoa burudani kwa mashabiki wa Wekundu wa Mzimbazi.

Hiki ndio kikosi cha Azam FC kwa ajili ya msimu ujao. Tukutane 2020/2021.

Alikiba akiendelea kuwapagawisha mashabiki
Alikiba akikonga nyoyo za mashabiki walioujaza uwanja wa Azam Complex
Mtangazaji wa kituo cha Azam TV, Baraka Mpenja akimiliki mpira kwenye mchezo uliowakutanisha wafanyakazi wa Azam Media dhidi ya Wanahabari FC
Mchezaji mpya wa Azam FC, Ayoub Lyanga
sehemu ya burudani katika tamasha hiloWachezaji wa Azam FC wakipongezana baada ya ushindi
Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza
Moja ya mikiki mikiki ya kuwania mpira katika mchezo huo
Msanii Alikiba akitoa burudani