Header Ads Widget

POLISI YAZUNGUMZIA AJALI YA BASI LA SABUNI EXPRESS ILIYOUA WATU 8 KAGERA

Basi la Sabuni Express lililopata ajali mkoani Kagera.

Watu Nane wamefariki Dunia na wengine 27 wamejeruhiwa, baada ya Basi la Sabuni Express lililokuwa likitoka Wilaya ya Muleba mkoani Kagera kuelekea mkoani Mwanza kupinduka katika kijiji cha Lutenge kilichoko wilayani Muleba.

Akizungumza na East Africa Television Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera Revocatus Malimi, amesema kuwa marehemu sita kati ya nane wamekwishatambuliwa na ndugu zao na kuwa miili yao imehifadhiwa katika Hospitali za Rubya na Ndolage zilizoko katika Wilaya hiyo.

Kamanda Malimi amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, ambapo ametaja majina ya marehemu waliotambulika na ndugu zao kuwa ni Justus Ruhoya, Philbert Katabazi, Paskazia Pastory, Vestina Clonery, Goleth Adolph na Prisca Revocatus ambaye ni mtoto wa mwezi mmoja, wote wakazi wa Wilaya ya Muleba.