Header Ads Widget

PICHA: WAGOMBEA UBUNGE CHADEMA, CUF JIMBO LA SOLWA NAO WACHUKUA FOMU

Mgombea Ubunge jimbo la Solwa mkoani Shinyanga kwa tiketi ya CHADEMA, Mwinula Washington Kasonzo (kulia) akionyesha fomu ya ubunge aliyokabidhiwa leo Agosti 20, 2020 na Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Hoja Mahiba (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
 Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Solwa, Hoja Mahiba (kushoto) akimkabidhi fomu ya ubunge, mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA, Mwinula Kasonzo leo Agosti 20, 2020 katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mgombe ubunge Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga kwa tiketi ya chama cha CUF, Aloyce Shija Shangaluka akionyesha fomu ya ubunge aliyochukua jana Agosti 19, 2020 katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimboni humo.
Bw. Shangaluka (kulia) akisaini fomu ya ubunge mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba ambaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo.
Bi. Hoja Mahiba akimkabidhi fomu Mgombea wa CUF, Aloyce Shangaluka

Picha kwa hisani ya Dhulkifl Sungura