Header Ads Widget

MWANA FA 'GWIJI', MENEJA WA DIAMOND PLATINUMZ WAPITISHWA UBUNGE CCM



Msanii Hamis Mwinjuma (Mwana FA)

Na Shinyanga Press Club
MIONGONI mwa majina ya wagombea ubunge yaliyopitiahwa leo Agosti 20, 2020 na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni la Msanii wa Muziki wa kizazi kipya maadhi ya kufoka foka (HipHop), Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA ambaye ameptishwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kukiwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu kwenye nafasi ya Ubunge jimbo Muheza mkoani Tanga.

Mwana FA amepitishwa na chama chake licha ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mchakato wa kura za maoni.

Mwingine kutoka tasnia ya burudani aliyepitishwa na CCM Kugombea ubunge ni Hamis Taletale maarufu kama BABU TALE, ambaye sasa ndiye mgombea wa ubunge Jimbo la Morogoro Mashariki mkoani Morogoro.

Licha ya kupitishwa leo na kamati kuu, Babu Tale pia ambaye ni Meneja wa Msanii wa Bongofleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz', alishinda kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho.
Hamis Taletale (Babu Tale)
 Babu Tale akiwa na Diamond Platinumz

Kupitishwa kwa wagombea hao kutoka tasnia ya Burudani na Muziki wa kizazi kipya nchini ni ongezeko la wasanii mbalimbali kutaka kuongeza nguvu bungeni, baada ya uwepo wa wasanii kama Joseph Mbilinyi maarufu kama SUGU ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Haule 'Profesa Jay' mbunge wa Mikumi, Vicky Kamata na Khadija Shaban 'Keisha'.