Header Ads Widget

TAZAMA PICHA: MAWAZIRI, VIONGOZI WA DINI NA WANASIASA MBALIMBALI WALIVYOCHUKUA FOMU ZA UBUNGE MAJIMBONI


Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, leo Julai 14, 2020, amechukua fomu ya kuomba ridhaa  ya chama chake ili kimteue kwa ajili ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kisarawe.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amechukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kupitia CCM leo Julai 14, 2020. Anayemkabidhi fomu hiyo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mbozi, Julius Mbwiga.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif  Mansoor Jamal, Leo amechukua fomu ya kuwania ubunge wa jimbo hilo.
Aliyekuwa Mlinzi wa zamani wa Baba wa Taifa ambaye pia alikuwa mlinzi mkuu wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa,  Aloyce Tendewa amechukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CCM.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako, leo Julai 14, 2020, amechukua fomu ya kuomba ridhaa chama chake ili kiweze kumteua, aweze kugombea Ubunge katika jimbo la Kasulu Mjini kupitia


  Fredrick Lowassa (Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa) leo amemkabidhiwa  fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM
Waziri wa Uwekezaji, Angellah Kairuki akichukua fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Same Magharibi kupitia CCM.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dkt. Angelina Mabula leo amechukua fomu ya kutetea kiti chake cha ubunge katika ofisi ya CCM wilaya ya Ilemela

Naibu Spika, Dkt.Tulia Ackson amechukua fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Mbeya mjini kupitia CCM.

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM. Jimbo hilo lilikuwa linaongozwa na Halima Mdee (Chadema).
Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, leo amechukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM.