Header Ads Widget

ORODHA WALIOCHUKUA FOMU YA UBUNGE SHINYANGA MJINI YAFIKA 30, YUMO MASELE NA GAKI

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Bashemu akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele.
 
 Orodha ya wanachama wa Chama Cha Mpainduzi (CCM) waliojitokeza leo kuchukua fomu za kuwania nafasi ya ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini mkoani Shinyanga imezidi kuongezeka na sasa imefika 30 kwa siku ya leo ya ufunguzi wa zoezi hilo.
Waliohitimisha orodha ya waliojitokeza leo ni Pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Stephen Masele (CCM) anayetetea kiti chake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Gaspar Kileo maarufu 'GAKI, Erasto Kwilasa, Mary Izengo na Jonathan Manyama.
 
Orodha ya waliochukua fomu kugombea ubunge Shinyanga Mjini kwa tiketi ya CCM
 
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Bashemu akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge, Gaspar Kileo (kulia).
  
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Gaspar Kileo amesema atazungumzia vipaumbele vyake mara baada ya chama chake kumpitisha kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.



Jonathan Manyama Kifunda akikabidhiwa fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM.