Header Ads Widget

RAIS WA BURUNDI KUPUNGUZA GHARAMA ZA SABUNI KUKABILIANA NA CORONA



Rais Evariste Ndayishimiye alitangaza hatua za kupambana na corona zinazotofautiana na za mtangulizi wake hayati Pierre Nkurunziza

Mamlaka nchini Burundi imetangaza kutumia njia za aina yake kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona na kuachana na namna ambavyo taifa hilo lilivyokuwa linakabiliana na janga hilo wakati wa utawala uliopita.
Katika hotuba yake mara baada ya kuapishwa urais, Bwana Evariste Ndayishimiye alitangaza hatua zifuatazo za kupambana na corona ikiwa ni pamoja na hatua maalum kuhusu matumizi ya sabuni.

Mosi ni kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya watu wanapata sabuni, gharama ya bidhaa hiyo inabidi ipungue kwa asilimia 50 huku serikali ikifidia nusu yake ili viwanda visipate hasara.
Aidha mtu yeyote atakayepatikana anauza sabuni kwa magendo kutoka Burundi atadhaniwa kuwa anasaidia kumbaza virusi vya corona na hivyo kuwajibishwa ipasavyo," alisema rais.
Katika miji yote, gharama ya maji itapunguzwa mpaka virusi vya corona vitakakapoisha.

Mtu yeyote atakayeonyesha dalili za ugonjwa wa corona atatakiwa kufika hospitalini na atatakiwa kupimwa na kuhudumiwa bure.
Kama mlipuko utaisha kila mtu atatakiwa kupima virusi hivyo.

Mabadiliko hayo yamekuja mara tu rais mpya Bwana Ndayishimiye alipoingia madarakani, licha ya kwamba wakati wa kampeni za urais wake picha mikusanyiko ya maelfu ya watu waliokusanyika katika mikutano ya kampeni za kisiasa ziliibua wasi wasi mkubwa wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona kabla ya taifa hilo kufanya uchaguzi tarehe 20 Mei mwaka huu.

Mikutano mikubwa ilishuhudiwa katika nchi hiyo ambapo tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ilitoa sabuni na ndoo kwa wagombea wa uchaguzi ilivitumiwe na wafuasi wao kunawa mikono wakati wa kampeni , wakati mmoja pia kemikali za kuua vimelea pia zilitumika.


Mikutano mikubwa ya uchaguzi iliyokusanya umati wa watu ilifanyika licha ya mlipuko wa virusi vya corona ambayo pia ilihudhuriwa na Bwana Ndayishimiye

Lakini "idadi ya watu waliohudhuria mikutano hiyo ilikuwa kubwa mno kiasi cha kutotoshwa na maji na vitakasa mikono vilivyokuwepo ", mmoja waliohudhuria mkutano wa kampeni katika mkoa wa Kirundo aliiambia BBC.

Mikutano mikubwa ya Kampeni za uchaguzi yaibua hofu ya maambukizi ya virusi vya corona.

Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu walielezea hofu zao huku wakiishutumu serikali kwa kuhatarisha maisha ya watu: