Header Ads Widget

EZEKIEL MAIGE AKWAMA JIMBO LA MSALALA, IDD KASSIM AIBUKA KIDEDEA






ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ameshindwa kwenye kura za maoni za kupata mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga.


Mshindi, Idd Kassim

Katika kura za maoni zilizopigwa leo Julai 21, 2020 mjini Kahama, mtia nia Iddi Kassim ameongoza kwa kupata kura 327 akifuatiwa na Ezekiel Maige anayetetea kiti hicho ambaye ameambulia kura 118, huku Khatib Mgeja akikusanya kura 75.
 
Ezekiel Maige

Ezekiel Maige amekuwa Mbunge wa Jimbo la Msalala kwa tiketi ya CCCM kwa kipindi cha miaka 15.