Header Ads Widget

LEMBELI ASHINDWA KUMZUIA KISHIMBA KAHAMA MJINI, AAMBULIA NAFASI YA TATU


 Jumanne Kishimba

ALIYEWAHI kuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini mkoani Shinyanga, James Lembeli ameshindwa kufua dafu mbele ya mbunge anayetetea nafasi yake, Jumanne Kishimba baada ya kubwagwa kwenye kura za maoni leo Julai 21, 2020.
 
Kishimba aliyekuwa anatetea kiti chake ameibuka mshindi kwenye kinyang'anyiro hicho cha kura za maoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata kura 234, Benjamini Ngaiwa amekuwa wa pili kwa kura 181, huku James Lembeli akiambulia kura 54 katika nafasi ya tatu.
James Lembeli