Header Ads Widget

ALIYESHINDA KURA ZA MAONI MBOGWE WAMTAKA KUJENGA DARAJA KUUNGANISHA KIJIJI CHA BUDODA NA NYAKASARUMA

Mshindi wa kura za maoni nafasi ya ubunge jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga akiomba kura kwa wajumbe was mkutano mkuu wa wilaya.

Na Shaban Njia        
MBOGWE

 WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita,wamemtaka Nicodemas Maganga baada ya kuchaguliwa na chama hicho kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo na kushinda anatakiwa kujenga  daraja litakalo unganisha mawasiliano ya Kijiji cha Budoda na Nyakasaruma

Walisema kuwa,daraja la Bododa kijiji cha Budoda limekuwa likikatika mara kwa mara hasa wakati wa Msimu wa Mvua za maska kuanza na kusababisha wananchi wa kijiji hicho na Nyakasaruma kukosa mawasiliano na wanawake wajawazito kushindwa kufika Hospitali kupata matibabu.

Wanachama waliyabainisha hayo jana wakati wakizungumza  kwa nyakati tofauti baada ya msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Geita David Azalia kumtangaza Nicodemas Maganga kuwa mshindi kwa kupata kura 265 dhidi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Augustino Masele aliyepata kura 212.

Asha Hamisi,mkazi wa kijiji cha Budoda kata ya Mbogwe alisema kuwa,kama chama kitampitisha Mganga kugombea nafasi ya ubunge na kufanikiwa kushinda anatakiwa kutatua changamo iliyopo ya mawasiliano ya daraja ya kijiji cha Budoda na Nyakasaruma ambayo imekuwa ikikatika wakati wa mvua za masika.

Nae Halima Abdu alisema kuwa,wakati wa mvua za masika baada ya daraja hilo kukatia endapo ikitokea mama mjamzito muda wake wa kujifungua umefika hulazimika kujifungulia nyumbani na kusababisha hali ya hatari juu ya mama na mtoto pale anapozalishwa na watu ambao si wataalamu.

Aidha alisema kuwa, kijiji hicho kina zahanati imejengwa kwa nguvu za wananchi na serikali na jengo limekamilika lakini hakuna wataalamu wala vifaa tiba na kusababisha kila mwaka wananchi kutembea umbali wa kilometa sita kwenda hospitali ya wilaya kutafuta matibabu.

Kwa Upande wake nicodemas Maganga aliyeshinda kura za maoni kwa kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mbogwe Augustino Masele alisema kuwa,akipata ridhaa na kushinda uchaguzi mkuu atahakikisha anajenga daraja la kisasa ili kuwepo kwa mawasiliano ya uhakika baina ya vijiji hivyo viwili.

Maganga aliongeza kuwa, Jimbo la Mbogwe lina changamoto nyingi sana ukilinganisha na majimbo yaliyoko Mkoni Geita na kuhaidi kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya ama zahanati ili kuwasogezea huduma za kiafya wananchi na kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto

 Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbogwe Bi Grace Shindika akihakiki karatasi za kura.
Wagombea 29 kati ya 31 waliochukua fomu za kuwania nafasi ya uwakilishi jimbo la Mbogwe wakionesha nambari zao za kupigia kura ili wajumbe wawapigie.