Header Ads Widget

JPM: MIMI SIYO MBINAFSI, ACHENI KUJENGA OFISI MBILI MBILI CHATO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameonyesha kushangazwa na kitendo cha Taasisi ya ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutaka kujenga ofisi nyingine wilayani Chato wakati tayari kulikuwa na ofisi alizoikabidhi taasisi hiyo.

Kitendo hicho kimemlazimu Rais Magufuli kusema kuwa yeye siyo mbinafsi kwani kitendo hicho kingetafsiriwa kwamba anapapendelea Chato ambako ni nyumbani kwao.

Na badala yake amependekeza fungu lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chato zipelekwe Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ambako hakuna ofisi ya Takukuru.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Julai 22, 2020 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi za Takukuru Wilaya ya Chamwino lenye thamani ya Sh Milioni 43.

Mbali na hayo, Rais Magufuli ameipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa iliyoifanya kwa kipindi cha miaka mitano.

"Nashangaa mnaniambia mnataka kujenga ofisi Chato wakati tayari kuna ofisi ya ghorofa na iko mlimani niliwakabidhi, mimi siyo mbinafsi msijenge ofisi mbili mbili Chato," amesema.