Header Ads Widget

UHASAMA KATI YA MAREKANI NA CHINA WAJITOKEZA KATIKA KUKABILIANA NA MLIPUKO WA CORONA AFRIKA.

Huku Afrika ikijiandaa kwa ongezeko la idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona , China na Marekani zinadai kuwa msaidizi mkubwa wa bara hili, lakini kuna mengi ambayo hayajaangaziwa katika uhasama huo zaidi ya kukabiliana na virusi hivyo.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba hakuna taifa litakaloshindana na kile ambacho Marekani inakifanya katika kusadia Afrika kukabiliana na Covid-19.
Na aliendelea kusema kwamba hakuna taifa ambalo limesaidia ama litafanya zaidi ya kusaidia Afya duniani.

Bwana Pompeo alikuwa akizungumza katika mkutano na kundi dogo la wanahabari wa Afrika pamoja na wale waliopiga kambi barani Afrika.

Wakati huo - mwezi uliopita - Nilichukulia tamko lake la 'hakuna taifa litakavyofanya zaidi', sawa na matamshi yanayotumiwa kila siku na utawala wa rais Trump, ambao ulikuwa unajaribu kuimarisha uhusiano wake wa kimataifa kufuatia uamuzi wake wa kukata uhusiano na Shirika la Afya Duniani WHO katikati ya mlipuko mkubwa zaidi duniani. Watoto walikuwa wakimkaribisha Ghana Mama wa taifa wa Marekani Melania Trump mwaka 2018.
Inasikitisha kusema kwamba $170m (£134m) za msaada ambazo bwana Pompeo anajigamba kuipatia Afrika zilishindwa na msaada wa bilionea mmoja wa China uliotolewa na Jack Ma.

lakini siku chache zilizopita, niliona habari kuhusu Afrika katika chombo kimoja cha habari kinachodhibitiwa na serikali, The global Times na nilikumbushwa kuhusu matamshi ya bwana Pompeo na kikanishangaza jinsi bara hili lilivyosukumwa katika kona moja ndogo ya vita baridi kati ya Washington na Beijing na kama ilivyokuwa awali katika vita vya baridi vilivyokuwa rasmi- mgogoro wa ghafla, kama ule wa virusi vya corona sasa umebadilishwa na kuwa mzozo fulani.
Habari hiyo ya Chombo cha habari cha Global Times ilijigamba kwamba mfumo wa China wa Kisiasa , ulifanikiwa katika kukabiliana na Virusi vya corona.

Na Baadaye likaendelea kusema kwamba huu ndio wakati ambao mataifa ya Afrika yanapaswa kusitisha utumizi wa mfumo wa vyama vingi unaotumiwa na mataifa ya magharibi.
 Mfumo ambao chombo hicho kinasema kwamba umesasabisha ukosefu wa usawa kikabila na kidini, ghasia uharibifu wa maisha na mali. 
Badala yake Afrika inapaswa kufuata mfumo wa chama kimoja wa China.