Header Ads Widget

RAIS WA MAREKANI ASEMA MKUTANO WA KAMPENI WA TULSA HAUKUHUDHURIWA NA UMATI WA WATU



Mkutano wa kampeni wa Trump ulifanyika mbele ya umati mdogo wa watu kuliko ilivyotarajiwa


Rais wa Marekani Donald Trump amefanya mkutano wake wa kwanza wa kampeni tangu nchi hiyo ilipoweka amri ya kutotoka nje kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, huku akiwa mbele ya watu wachache badala ya umati mkubwa wa watu uliotarajiwa.
Bwana Trump alikua amejigamba mapema wiki hii kwamba karibu watu milioni walikua wameomba tiketi za kuhudhuuria mkutano huo katika eneo la benki ya Tulsa katika kituo cha Oklahoma.

Lakini viti 19,000 vya uwanja huo viliachwa wazi bila watu na mipango yake ya kuhutubia watu ambao alitarajia wangelazimika kukaa nje iwapo uwanja ungefurika ilibidi iachwe.

Kumekua na hofu juu ya kuendesha mikutano ya kisiasa wakati wa janga la corona.

Virusi vya corona lilikua ni suala moja lililozungumziwa na Bwana Trump katika mkutano huo, katika hotuba yake iliyodumu karibu saa mbili kwa wafuasi wake waliokua wakimshangilia, katika eneo hilo ambalo ni kitovu cha Republican.

Bwana Trump alisema kuwa aliwaambia maafisa kupunguza upimaji wa virusi vya Covid-19 kwasababu watu wengi sana walikua wanapatikana na virusi, lakini baadae katika hotuba hiyo akasema maneno hayo ni mzaha tu.

Wale waliohudhuria mkutano wa kampeni walilazimika kusaini makubaliano ya kuilinda timu ya kampeni ya Trump kwamba haitawajibika na ugonjwa wowote iwapo watapata maambukizi. Saa kadhaa kabla ya tukio hilo kuanza, maafisa walisema kuwa wahudumu sita wa kampeni ya Trump walipatikana na maambukizi ya virusi vya corona.


Hatahivyo, haijawa wazi ni kwanini ni watu wachache waliojitokeza kuliko ilivyotarajiwa. Bwana Trump aliwaelezea wale waliokuwa uwanjani kumsikiliza kama "wapiganaji", huku akiwalaumu waandamanaji na vyombo vya habari kwa kuwafukuza wafuasi wake. Kulikua na kizaazaa nje ya uwanja wa mkutano, lakini hapakua na matatizo makubwa yaliyojitokeza.

Wafuasi wengi wa Trump hawakua wamevaa barakoa katika mkutano wa kampeni

Kampeni za Trump za kuwania kuchaguliwa tena kama rais wa Marekani zilikua ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu katika eneo lililofungwa kuwahi kushuhudiwa tangu Marekani ilipotangaza mlipuko wa Covid-19, na unafanyika wakati Oklahoma ikishuhudia ongezeko la visa vya corona vilivyothibitishwa.

Zaidi ya wagonjwa milioni 22 wa Covid-19 na vifo 119,000 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa nchini Marekani, kwa mujibu wa data kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Katika hotuba yake ya ufunguzi , Bwana Trump alisema kuwa kumekua na "watu wabaya sana nje, wanafanya vitu vibaya sana", lakini hakufafanua zaidi. Wanaharakati wa Black Lives Matter walikua ni miongoni mwa waandamanaji waliokua wamekusanyioka nje ya uwanja wa kampeni ya Trump kupinga mkutano huo kabla kampeni hazijaanza.


Kuhusu virusi vya corona, Bwana Trump aliwatia moyo maafisa kupunguza kasi ya kupima virusi kwasababu ilisababisha kugunduliwa kwa watu wengi wenye virusi.



Waliohudhuria walisaini makubaliano ya kuilinda kampeni ya Trump dhidi ya kuwajibika kwa ugonjwa wowote ule

"Huu ndio ubaya: Unapofanya vipimo kwa kiasi kile, utawapata watu wengi, utapata visa vingi vya corona, aliuambia umati wa wafuasi wake uliomshangilia . "Kwahiyo nikasema 'punguza kasi ya kupima'. Walipima na wakapima."

Trump alisema kuwa, virusi vya corona, vilikua na majina mengi likiwemo "Kung Flu", neno la ubaguzi ambalo linaielezea China, ambako Covid-19 ulianzia.

Takriban watu 120,000 wameuawa na Covid-19 nchini Marekani tangu janga lilipoanza, idadi ambayo wataalamu wa afya wanasema ingekua juu zaidi kama upimaji wa virusi hivyo usingefanyika. Maafisa wa afya wanasema upimaji ni muhimu ili kuelewa ni wapi na ni kwa vipi virusi vya corona vinasambaa, na hivyo kuzuwia vifo zaidi


Maafisa wa Ikulu ya White House baadae walisema kuwa ''bila shaka rais alikua akitoa mzaha " kuhusu kupima Covid-19.

Rais Trump Donald alikejeli upimaji wa virusi vya corona Marekani

Akimzungumzia hasimu wake , mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic, Bwana Trump alimuelezea Joe Biden kama "mtu aliyeweza kujisimamia na kibonzo cha itikadi kali za mrengo wa kushoto ".

Rais pia alionekana kuwa mwenye ghadhabu alipozungumzia maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na kuangushwa kwa sanamu -ambako kulianza baada ya mauaji ya mtu mweusi aliyejulikana , George Floyd, yaliyotekelezwa na pilisi wa Minneapolis.

"Jengela mrengo wa kushoto linajaribu kuharibu historia yetu, kuharibu minara yetu-minara yetu mizuri-kuangusha minara yetu na kuadhibu, kumhukumu kila mtu ambaye hakubaliani na madai yao ya kupata udhibiti kamili.