Header Ads Widget

MFUMO BORA WA KUTAINI KUSAIDIA KUEPUSHA RUSHWA YA NGONO VYUONI




KUTOKANA na kubainika kuwepo kwa rushwa ya ngono, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amevitaka Vyuo vyote vya Elimu ya Juu kuweka utaratibu wa namna bora ya kutahini wanavyuo pale wanapokuwa wanawadahili kwa kuwapima uwezo wao ili kuepuka rushwa ya ngono.
Dkt. Mahenge ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifungua semina ya siku moja kwa wanavyuo mbalimbali mkoani hapa yanayohusu rushwa ya ngono na namna wanafunzi hao wataweza kuepukana nayo .

Amesema, kutokana na tafiti za wataalam zilizofanywa katika Vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma zimeonyesha kuwa wanavyuo wengi hasa wa kike wamekuwa wakiwashawishi wahadhiri wanaume kwa njia ya ngono ili waweze kufaulu mitihani yao.

“Kumekuwepo na baadhi ya wanavyuo kuwashawishi walimu wao kingono kwakutumia miili yao ili waweze kufaulu mitihani yao jambo ambalo si jema kabisa, na hata tukiamua tutoe makaratasi kwa wanavyuo ili walioshiriki wavitaje vyuo ambavyo vinaongoza kutokana na vitendo hivyo tutavipata vingi, hivyo inabidi tuanze kupinga vitendo hivi,” amesisitiza Dkt. Mahenge

Amesema, ukosefu wa maadili ikiwa ni pamoja ulevi na kukosa heshima ni moja ya sababu zinazochangia kuwepo kwa vitendo hivyo vya rushwa na kuathiri vyuo kwa namna mbalimbli na kupelekea kupata wataalam wasiokuwa na uwezo katika utendaji kazi wao.

Hata hivyo ametaka ufike wakati kila Taasisi kuhakikisha inasimamaia suala hilo kwa kulipinga na kulikemea kwani likiachwa liendelee lazima Taifa litapata wataalam wasiokuwa na uwezo.

Pia ameiagiza Takukuru kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na viongozi wa Vyuo kupitia klabu za kupambana na rushwa katika taasisi hizo za elimu ya juu ili kuweza kukemea vitendo hivyo.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo amesema, kutokana na Taasisi hiyo kupokea malalamiko dhidi ya rushwa ya ngono tayari wameshafungua jumla ya majalada 23 kuhusiana na rushwa ya ngono toka mwaka 2013 huku kesi 10 zikiwa tayari zimeshafikishwa Mahakamni.

“Rushwa ya ngono katika Taasisi za elimu ya juu imeonekana kuwa ni tatizo ndio maana kama Taasisi katika kukabiliana nalo tumeamua kuanzisha mafunzo lengo kiliwa ni kutokomeza na kumaliza kabisa vitendo hivyo,” amesema mkuu huyo.

Imebainika kuwa, katika Vyuo vikuu asilimia 68 ya wahadhiri walitoa maoni yao na kukiri kuwepo kwa tatizo hilo huku asilimia 57 ya wanavyuo wakikiri kuwepo kwa tatizo hilo la rushwa ya ngono.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango, Taaluma Dkt. Proventi Dimoso amesema kuwa, vitendo vya rushwkoa ya ngono ndani yake kumekuwa na udhalilishaji na hupeleka watu kuathirika kisaikolojia hivyo anaamini semina hiyo itakuwa chachu ya mabadili