Header Ads Widget

CUF YAVUNA WANACHAMA ZAIDI YA 500 KUTOKA CHAMA CHA ACT -WAZALENDO

 
Wanachama zaidi ya 300 wa chama cha ACT wazalendo wa jimbo la Ziwani na Wawi warejesha kadi za ACT na kuendelea kutumikia chama chao cha CUF na kueleza kuwa hawako tayari kuidhulumu mioyo yao kutumikia ACT badala yake wataendelea kubaki CUF waliyotoka nayo mbali tokea miaka 27 iliyopita.

Zaidi ya wananchi 500 wa Jimbo la Ziwani na Wawi visiwani Pemba wamerejesha kadi za Chama cha ACT Wazalendo mbele ya wenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na kusema kuwa wao ni wafuasi wa CUF kwa miaka zaidi ya 27 na si wafuasi wa ACT Wazalendo.



Pia wananchi hao wamemlilia Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kufuatia ubovu mkubwa wa barabara unaowakabili kwa kipindi kirefu sasa na kuomba pindi watakapowapa ridhaa ya kuingia kwenye Serikali ya kitaifa waweze kuwatatulia kero hiyo.

Wananchi hao wametoa kilio hicho wakati Mwenyekiti huyo wa CUF alipokuwa akizindua moja ya tawi la Bilikau kwenye ziara yake ya kichama visiwani humo.

Seleman Jumaa ni mmoja wa wananchi hao ambaye amesema, kila wanaposikia nyimbo za chama cha CUF nafsi zimekuwa zikiwauma sana na kujiona kwa nini watumikie ACT, chama ambacho hakijawatoa mbali.

”Mheshimiwa Mwenyekiti Lipumba mimi binafsi niliposikia hii nyimbo tu ya CUF imenikumbusha mbali sana na kujiona mkosaji kuhama CUF, leo hii nakukabidhi kadi hizi za wananchi wengi waliokwenda ACT wamesema wanataka kurudi nyumbani kwenye chama chao,”amesisitiza Jumaa.

Kwa upande wake mtia nia ubunge jimbo hilo, Mbaruk Seif Salum amesema, ameamua kugombea jimbo hilo kwa kuwa wabunge wengi waliopita si wakweli kwani wakipewa ridhaa wanawasahau wananchi.