Picha mbalimbali zikimuonesha Rashford akiwa anafanya mazoezi leo kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Aon Training Complex
Na Damian Masyenene na Mitandao
Habari Njema kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United ya Uingereza baada ya Mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashford kurejea mazoezini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitano kutokana na majeraha ya mgongo.
Rashford ambaye ndiye kinara wa mabao msimu huu ndani ya klabu hiyo akiwa amefunga mabao 19 katika mashindano yote alipata majeraha mwishoni mwa mwaka jana na kulazimika kukosa michezo 13 ya timu hiyo.
kwa mujibu wa picha zilizochapishwa katika tovuti ya klabu ya Manchester United leo Mei 22, 2020 imemuonyesha Muingereza huyo akiwa anafanya mazoezi peke yake chini ya uangalizi (hakujumuika na wenzake) katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo, AON Training Complex.
Hata hivyo, haijaelezwa bayana ni lini mshambuliaji huyo ataungana na wenzake kuanza kuwatumikia mashetani hao wekendu. Rashford ameshaitumikia Manchester United michezo 201 hivyo kurejea kwake uwanjani na kuitumikia timu yake kutamfanya kuwa mchezaji wa 99 kuitumkia United michezo mingi akiwa juu ya mkongwe Gordon Strachan.