Header Ads Widget

AGAPE WATOA ELIMU YA UKATILI, CORONA MWAMALA



Shirika la Agape ambalo linatetea haki za watoto mkoani Shinyanga, limetoa elimu ya ukatili na jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kwa wajumbe wa kamati ya Mtakuwwa Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Elimu hiyo imetolewa leo Mei 22, 2020 katika ofisi ya Kata ya Mwamala kwa kukutana na wajumbe wa mpango mkakati wa Serikali wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (Mtakuwwa)Kata hiyo ya Mwamala.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, amesema katika kipindi hiki cha janga la maambukizi ya virusi vya Corona, wameamua kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi hayo sambamba na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa ufadhili wa Shirika la Mundo Cooparante.

Amesema Shirika kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wanatoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona katika maeneo ya vijijini pamoja na elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, ili jamii ibaki kuwa salama.

"Shirika letu la Agape tunaungana na Serikali kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na kupinga matukio ya ukatili katika maeneo ya vijijini, na sasa tupo Kata ya Mwamala pamoja na kutoa vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo zikiwamo ndoo za majitiririka na sabuni," amesema Myola.

Naye Afisa maendeleo Kata ya Mwamala Sophia Philbert, ambaye pia ni katibu wa Mtakuwwa, amewataka wajumbe hao kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi katika kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona, pamoja kuimarisha ulinzi dhidi ya watoto na kuwazuia kuzurura hovyo.

Kwa upande wake mhudumu wa afya katika kituo cha Samuye, Ilambona Alfred, ametoa elimu kwa wajumbe hao namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na majitiririka, kukaa umbali wa mita moja, kuvaa barakoa, pamoja na kutokaa kwenye makundi.

Aidha afisa tarafa wa Samuye Ntarle Magese, ametoa wito kwa wananchi kuacha kupuuzia janga hilo la maambukizi ya virusi vya Corona licha ya kupungua, bali waendelee kuchukua tahadhari hadi pale Serikali itakapo tangaza janga hilo limeisha hapa nchini.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, akitoa elimu ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa wajumbe wa kamati ya Mtakuwwa Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akiendelea kutoa elimu ya kupinga ukatili kwa wajumbe wa Kamati ya Mtakuwwa Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Afisa maendeleo Kata ya Mwamala Sophia Philbert, ambaye pia ni Katibu wa Mtakuwwa, akitoa elimu kwa wajumbe wa Kamati ya Mtakuwwa namna ya kutekeleza majukumu yao katika kupambana kupunguza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Mhudumu wa afya kutoka kituo cha afya Samuye Ilambona Alfred, akitoa elimu namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Afisa tarafa ya Samuye Ntarle Magese, akisisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona licha ya kupungua.

Diwani wa kata ya Mwamala Hamisi, akipongeza Shirika hilo la Agape kwa kuendelea kuhudumia jamii kwa kutoa elimu ya Corona pamoja na vifaa sanjari na elimu ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Afisa mradi wa kutokomeza ndoa za utotoni na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutoka Shirika la Agape Sophia Rwazo, akiwasihi wajumbe wa kamati ya Mtakuwwa Mwamala, wachape kazi kwa kushirikiana ili waweze kutimiza malengo ya kupunguza ukatili ndani ya jamii.

Wajumbe wa Mtakuwwa Mwamala wakiwa kwenye kikao.


Wajumbe wakiendelea na kikao.


Mjumbe wa Kamati ya Mtakuwwa Salome Ndaki akichangia mada.


Mjumbe wa kamati ya Mtakuwwa Boniphace Boazi akichangia mada.


Mjumbe wa kamati ya Mtakuwwa Ramadhani Dotto akichangia mada.

Mratibu wa miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani akishusha vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona tayari kwa kuvigawa Mwamala.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, akitoa elimu namna ya kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa wajumbe wa kamati ya Mtakuwwa kabla ya kuvigawa.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola, wakwanza kulia, akitoa maelezo wakati wa kukabidhii kifaa cha kisasa cha kunawa mikono kwa Sabuni na majitiririka kwa wajumbe wa Mtakuwwa ambacho kitaweka kwenye kituo cha afya Bogogo ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Zoezi la upokeaji vifaa vya kisasa ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona likiendelea, ambapo kifaa hicho kitapelekwa kituo cha afya Mwamala.

Zoezi la upokeaji vifaa vya kisasa ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona likiendelea, ambapo kifaa hicho kitawekwa kwenye ofisi ya Kata ya Mwamala.

Diwani wa Kata ya Mwamala Hamisi Masanja akinawa mikono kwa sabuni na majitiririka mara baada ya kumaliza kukabidhiwa kifaa hicho na Shirika la Agape kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.

Afisa mtendaji wa Kata ya Mwamala Suzani Kayange, akinawa mikono kwa sabuni na majitiririka mara baada ya kumaliza kukabidhiwa kifaa cha kisasa na Shirika la Agape ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo John Myola.

Afisa tarafa Samuye Ntarle Magese naye akinawa mikono kwa sabuni na majitiririka.


Shehe Ramadhani Dotto,akinawa mikono kwa sabuni na majitiririka.
Picha zote na Marco Maduhu.