Header Ads Widget

CWT KAHAMA YAPATA MWENYEKTI MPYA AWATAKA WALIMU KUSHIRIKIANA


Mwenyekiti mpya wa Chama cha Walimu wilaya ya Kahama(CWT) Raymond Yothamu Lutemba akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu baada ya kumchagua kukiongoza chama hicho.Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha walimu wilaya ya Kahama wakiwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika katika viwanja vya ofisi yao ya wilaya.

Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Shinyanga (CWT)Lazaro Saulo  ambae alikuwa msimamia  mkuu wa uchaguzi wa  (CWT), kulia kwake ni  mwenyekiti wa uchaguzi huo Gregory Mazoya.

Aliyekuwa mwenyekiti wa CWT wilaya ya Kahama Edina Kalambo aliyekaa kushoto baada ya kushindwa katika uchaguzi huo kwa kupata kura 72, akiwa na mwenyekiti mpya wa CWT Raymond Yothamu Lutemba aliyeshinda kwa kura 111.

Na Patrick Mabula,Kahama

Mkutano mkuu wa chama cha walimu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umemchagua Raymond Lutemba kuwa mwenyekiti wa chama hicho baada ya kuwashinda wagombea wenzake sita kwa kupata kura 111.

 Katika uchaguzi huo uliofanyika viwanja vya ofisi ya CWT wlaya ya Kahama ambao ulikuwa na ushindani mkubwa, huku Edina Kalambo aliyekuwa anatetea nafasi yake alipata kura 72 akifuatiwa na Machege Emmanuel akipata kura 14. 

Wengine waliokuwa wanawania nafasi hiyo ya mwenyekiti alikuwa ni Otieno Thomas 10,Cleophace Hilderphonce 1,Jucael Mpanda 1 na Godfrey Harmas 0 ambao kwa pamoja walikubaliana na matokeo ya uchaguzi.

Kwa upande wa nafasi ya uweka hazina ambayo ilikuwa na wagombea watano,aliyechaguliwa ni Werema Michael aliyepata kura 114 wengine ni Samwel Luhende 61 , Samson Mwesigwa 9 , Elisha Mhoja 2 na Martin Mgonga aliyejipatia kula 24.

Nafasi za  wajumbe wa kamati tendaji waliochaguliwa ni Shija Sulugwayi vijana, Paul Mlele wenye ulemavu, Polina Aporinali wanawake, Hema Modestus taasisi na uongozi, Luhamba Mwamini shule za awali.

Wengine ni Mwita Agustino na Kabadi Ilemela shule za sekondari  na wawakilishi wa shule za msingi ni Mhoja Ramadhani , Mwamini Mhamsis ,Kado Kizito na Deusdetit Ntobi.

Akiongea baada ya kuchaguliwa mwenyekiti mpya wa CWT wilaya ya Kahama aliwataka walimu kudumisha mshikamano huku akibainsha kuwa atahakikisha anatetea maslahi yao pamoja na kusimamia  kupandishwa madaraja kwa wakati ili haki iweze kuonekana wanapotimiza wajibu wao wa kazi.

TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807