` WAZIRI KAPINGA ASHIRIKI HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA KICHUNGAJI CHA VIJANA MBINGA

WANDAMAN HOTEL

WAZIRI KAPINGA ASHIRIKI HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA KICHUNGAJI CHA VIJANA MBINGA

   

📌Aungana na Wadau wake achangisha zaidi ya Mil.124 za ujenzi wa Kituo cha Kichungaji.

📌Ahimiza kuwa Kanisa ni Msingi Muhimu wa Malezi na Uimarishaji wa maadili.
**
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb) amesema kanisa lina nafasi muhimu katika kuimarisha malezi na maadili ya jamii, hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto ya mmomonyoko wa maadili.

Kapinga ametoa kauli hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kichungaji cha Vijana Jimbo katholiki la Mbinga, Novemba 19,2026, mkoani Ruvuma

Katika harambee hiyo, Waziri Kapinga ameungana na baadhi ya Viongozi wadau wa Jimbo na marafiki na kufanikiwa kuchangisha zaidi ya Sh milioni 124 na kujumuisha na michango ya waumini wa kanisa na kufanikiwa kupatikana jumla ya sh. Milioni 440 ambapo fedha hizo zinazolenga kusaidia ujenzi wa kituo hicho cha kichungaji kwa ajili ya vijana ambapo bajeti yake inakadiriwa kuwa zaidi ya Bilioni 1.

Amesema taasisi za dini, hususan Kanisa Katholiki, zina mchango mkubwa katika kujenga jamii yenye maadili mema kupitia mafundisho, malezi na ushauri unaotolewa kwa waumini na vijana.

Amesisitiza kuwa waumini wa Kanisa Katoliki wana wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kulisaidia kanisa kutekeleza majukumu yake, ikiwemo kuimarisha malezi ya vijana na kuwajenga katika misingi bora ya maisha.

Aidha, amesema ataendelea kuwa sehemu ya kusaidia na kuunga mkono masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha huduma na shughuli za kanisa, akieleza kuwa ushiriki katika mambo hayo ni muhimu kwa maendeleo ya jamii.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464