` SBC PEPSI YANOGESHA HAFLA YA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

WANDAMAN HOTEL

SBC PEPSI YANOGESHA HAFLA YA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

 


SBC Pepsi Yanogesha Hafla ya Waandishi wa Habari Mwanza

Mwandishi wetu

Mwanza

Wahariri na waandishi wa habari ambao ni wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA Tanzania), wameishukuru Kampuni ya SBC kwa kuwa miongoni mwa wafadhili wakubwa walionogesha hafla ya jioni iliyowakutanisha waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa taasisi hiyo jijini Mwanza.


Hafla hiyo ilifana kwa kushirikisha zaidi ya waandishi wa habari 60 ambao ni wanachama wa MISA Tanzania, pamoja na wadau mbalimbali waliokutana kwa lengo la kuimarisha mahusiano, kuendeleza ushirikiano na kutambua mchango wa wadau katika sekta ya habari nchini.
Ufadhili wa Kampuni ya SBC ulikuwa sehemu muhimu ya kufanikisha hafla hiyo, huku mchango wake ukionekana kuwa kielelezo cha ushirikiano mzuri kati ya sekta binafsi na vyombo vya habari.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edqwin Soko, alitoa shukrani kwa Kampuni ya SBC kwa kukubali kuwa miongoni mwa wafadhili wa hafla ya jioni ya wadau wa MISA Tanzania.

Soko aliishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono hafla hiyo na kutambua umuhimu wa kushirikiana na wanahabari, ambao wana jukumu kubwa la kuhabarisha umma na kuchangia maendeleo ya jamii.
Aidha, Mwenyekiti huyo alitoa shukrani za pekee kwa Bwana Arun Kumar, Afisa Masoko, na Bwana Joseph Sospeter, Msimamizi wa Kampuni ya SBC, kwa kuendeleza mahusiano mazuri na vyombo vya habari.

Alieleza kuwa ushirikiano kati ya kampuni na wanahabari ni muhimu katika kujenga mazingira mazuri ya mawasiliano, kuimarisha uhusiano wa wadau na kuwezesha shughuli mbalimbali zinazowakutanisha wanahabari na taasisi zinazounga mkono maendeleo ya sekta ya habari.

Kwa upande wao, wanachama wa MISA Tanzania walitambua mchango wa SBC katika kufanikisha hafla hiyo, wakieleza kuwa ushiriki wa kampuni hiyo ni ishara ya kuthamini nafasi ya waandishi wa habari na umuhimu wa kujenga ushirikiano endelevu kati ya vyombo vya habari na sekta binafsi.

Hafla hiyo pia ilitoa fursa kwa waandishi wa habari na wadau wengine kubadilishana mawazo, kuimarisha mitandao ya mawasiliano na kujenga mahusiano yatakayosaidia kuendeleza ushirikiano katika shughuli zao za kila siku.

Kwa kushirikisha zaidi ya waandishi wa habari 60 na wadau mbalimbali, hafla hiyo imekuwa sehemu muhimu ya kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanachama wa MISA Tanzania na kutambua mchango wa washirika wanaounga mkono shughuli za taasisi hiyo.

Mchango wa Kampuni ya SBC umeendelea kuonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na vyombo vya habari katika kuandaa matukio yanayowakutanisha wadau, kuimarisha mahusiano na kukuza ushirikiano kwa manufaa ya sekta ya habari nchini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464