` MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA SETH MSANGWA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI MBEGU ZA KILIMO KWA WAKULIMA

WANDAMAN HOTEL

MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA SETH MSANGWA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI MBEGU ZA KILIMO KWA WAKULIMA


MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA SETH MSANGWA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI MBEGU ZA KILIMO KWA WAKULIMA

********

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Seth Msangwa, amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa mbegu bora za alizeti na mpunga kwa wakulima kwa msimu wa kilimo wa 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuongeza tija katika uzalishaji.
TAZAMA VIDEO👇👇


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Msangwa amesema ugawaji wa mbegu hizo unalenga kuwasaidia wakulima kuwa tayari kukabiliana na changamoto za msimu wa mvua unaotarajiwa, hususani katika maeneo yanayoweza kuathiriwa na mabadiliko ya mwenendo wa mvua.
Aidha, Mhe. Msangwa amewataka wananchi kutumia mbegu hizo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na kupata ushauri kutoka kwa maafisa ugani wa kilimo ili kuhakikisha wanapata tija na mavuno bora.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Godfrey Mbwambo, amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, Halmashauri ilipanga kununua jumla ya tani 2.7 za mbegu bora za mpunga pamoja na tani moja ya mbegu bora za alizeti, ambazo zinatarajiwa kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kuwa na uhakika zaidi wa mavuno, huku wakizingatia mbinu bora za kilimo zinazokabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Mhandisi Mbwambo ameongeza kuwa zoezi la ugawaji wa mbegu ni miongoni mwa hatua zinazolenga kuimarisha uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, pamoja na kuongeza kipato cha wakulima katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Ugawaji wa mbegu ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza sekta ya kilimo na kutekeleza ajenda ya kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa, ikiwemo kufikia azma ya 10/30, ambapo kilimo kinatarajiwa kuchangia asilimia 10 ya uchumi ifikapo mwaka 2030.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464