` RC MHITA AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA YA KAHAMA FRANCIS DAUDI MLACHA

WANDAMAN HOTEL

RC MHITA AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA YA KAHAMA FRANCIS DAUDI MLACHA

 


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amemuapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Dk. Francis Daud Mlacha, huku akitoa maagizo kwa wakuu wa wilaya ya mkoa huo, kuendelea kusikiliza kero za wananchi, kusimamia miradi ya maendeleo na halmashauri.

TAZAMA VIDEO YA UAPISHO👇👇


Hafla ya uapisho huo umefanyika leo Oktoba 5,2026 katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
Mboni, akizungumza wakati wa uapisho huo, kwanza amempongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kuaminiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kuwa mkuu mpya wa wilaya ya Kahama na kumsihi akachape kazi kwa bidii na kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama.

“Nakupogeza sana kwa kuteuliwa na Rais wetu kuwa Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama, karibu Shinyanga kwenye timu ya ushindi,” amesema Mhita.
Aidha, ametoa pia maelekezo kwa wakurugenzi wa Halmashauri sita za mkoa huo , kwamba waongeze kasi ya ukusanyaji mapato, kuibua vyanzo vipya, pamoja na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato hayo.
Maagizo mengine ni kutenga bajeti kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imekuwa ikianzishwa kwa nguvu za wananchi, pamoja na kulipa madeni ya wazabuni na kutozalisha madeni mapya.
Amesisitiza pia kusimamiwa kwa zoezi la usafi wa mazingira ikiwamo kuzibua mitaro katika kukabiliana na athari za mvua za El Nino.

Kwa upande wake Mkuu huyo mpya wa wilaya ya Kahama Dk. Francis Daudi Mlacha, ameshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama, ambapo ameahidi kuchapa kazi na kutekeleza maagizo yote.
Amesema, jambo la kwamba ambalo ataanza nalo katika wilaya hiyo ya Kahama ni changamoto ya ubovu wa miundombinu ya barabara pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato na kudhibiti matumizi yake.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Dk. Francis Daudi Mlacha akiapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita.
Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Dk. Francis Daudi Mlacha akiapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita.
Mkuu mpya wa wilaya ya Kahama Dk. Francis Daudi Mlacha akiapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464