` MTU MMOJA AKAMATWA NA POLISI KWA KUMSHAMBULIA KWA NGUMI NA MATEKE ASKARI

WANDAMAN HOTEL

MTU MMOJA AKAMATWA NA POLISI KWA KUMSHAMBULIA KWA NGUMI NA MATEKE ASKARI


Jeshi la Polisi Dar es Salaam linamshikilia Conrad Agonza Kayoza, mwenye umri wa miaka 35, kwa tuhuma za kumshambulia kwa ngumi na mateke askari wa Usalama Barabarani aliyekuwa akitekeleza majukumu yake eneo la Lugalo, Kinondoni.


Tukio hilo limetokea leo Septemba 8, 2026, majira ya saa 1:30 asubuhi katika Barabara ya Bagamoyo, ambapo Askari Polisi namba F.8886 SGT Andrew aliwaelekeza madereva kutotumia Service Road nje ya utaratibu, ikiwemo gari aina ya Toyota Runx lenye namba T 455 EER.

Polisi imesema baada ya kusimamishwa, Conrad alishuka kwenye gari na kuanza kumshambulia askari huyo. Baadaye mtuhumiwa naye alishambuliwa na wananchi waliokuwa eneo hilo, kabla ya kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Jeshi la Polisi limesema mtuhumiwa atahojiwa kwa kina baada ya kupata nafuu ili hatua za kisheria zichukuliwe, huku likitoa onyo kali kuwa halitasita kuchukua hatua dhidi ya mtu au kundi lolote litakalowashambulia askari wakati wakitekeleza majukumu yao.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464