Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
Maafisa usafi Manispaa ya Shinyanga, wameiomba kulipwa malimbizo ya madai yao, wakisema hatua hiyo itawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi kwa kuhakikisha mji huo unaendelea kuwa katika hali ya usafi.
Wamebainisha hayo jana kwenyem kupitia Risala yao iliyosomwa na Afisa Usafi Amos Paul, katika kikao cha maafisa usafi wa Manispaa ya Shinyanga.
Paul amesema, pamoja na malimbikizo ya madeni yao bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo ya ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kukusanyia na kuzoa taka, hali inayofanya kazi yao kuwa ngumu.
Aidha, amesema changamoto nyingine ambayo wanakabiliana na nayo ni katika mfumo wa TAUSI pamoja na hitilafu za mifumo ya benki, ambao zimeathiri ukusanyaji na uwasilishaji wa mapato, hasa katika kipindi cha mwezi Agost na Septemba.
“Changamoto za mifumo zimekuwa zikikwamisha uksanyaji wa mapato,” amesema Paul.
Mkurugenzi wa ATA Safari and Lodges na mdau wa usafi Alfred Mlahi, amewaomba wadau wa mazingira na usafi, kushirikiana katika kuwapatia vifaa vya usalama, ikiwemo “Reflector” kwa wafanya usafi, hasa wanaofanya kazi za kufagia barabarani.
Amesema ,vifaa hivyo vitasaidia kuongeza usalama wao wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Pia amewataka wananchi kupewa elimu kuhusu ulipaji wa ushuru, ili waweze kulipa kwa wakati na kwa hiari, hatua ambayo itasaidia maafisa usafi kupata stahiki zao kwa wakati na kuongeza mapato ya Manispaa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mgeni Rasmi katika kikao hicho, ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salumu Kitumbo, amesema atahakikisha maafisa usafi wenye malimbizo ya madai wanalipwa kwa wakati.
Amesema, pamoja na malipo hayo, ataendelea kushirikiana na wahusika kuhakikisha maafisa hao wanapata stahiki zao kwa wakati, ili waweze kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Nasoro Walioba, amesema Mtaa huo, umeshika nafasi ya tatu kwa usafi nchini Tanzania, kutokana na juhudi zinazofanywa na maafisa usafi wa Manispaa hiyo.
Amesema, mafanikio hayo yanaonesha umuhimu wa kuendelea kuwaunga mkono wafanyakazi wanaohusika na usafi wa mazingira.
Katika kuunga mkono juhudi za kukabiliana na changamoto za usafi, mdau wa mazingira Salum Abeid, amechangia vifaa vya usafi vikiwemo “Reflector” 50, na kuahidi kutoa Toroli mbili za kuzoa taka.
Ameasema, msaada huo unalenga kuongeza uwezo wa maafisa usafi, katika ukusanyaji wa taka na kuboresha mazingira ya Manispaa ya Shinyanga.
Naye Mwakilishi wa Networking Youth group Vitalis Bernard Alley, amesema siku ya leo wamejipa thamani baada ya kuona kuwa hawajapewa thamani kutokana na kazi ngumu wanayoifanya kwa zaidi ya miaka kadhaa.
Amesema wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa bidii ili kuhakikisha wanapata mahitaji yao ya msingi, ikiwamo chakula, huku wakimuomba Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga kuwa mlezi wao, na kuwawakilisha katika changamoto wanazokabiliana nazo.
Amesema, malipo yao yanapitia Halmashauri, hivyo amemuomba Mstahiki Meya awapiganie ili watambuliwe na kuthaminiwa na wadau, pamoja na kusaidiwa kupata vifaa vya kisasa vitakavyowawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Aidha, amewaomba viongozi kuhakikisha akina baba na mama wanaofanya kazi kwenye mitaro, wanawahi kulipwa stahiki zao, kwa kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu na yenye changamoto.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwakilishi wa Networking Youth group Vitalis Bernard Alley akizungumza.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Salum Kitumbo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Nassoro Warioba akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464