SHULE YA HOPE YAJIVUNIA UFAULU, YATOA UHAKIKA WA USALAMA WANAFUNZI KIPINDI CHA MVUA ZA EL NIÑO
Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
Shule ya Msingi ya English Medium and Primary Schoo Hope imejivunia ufaulu mzuri wa wanafunzi wake, huku ikiwahakikishia wazazi kuwa imejipanga kuhakikisha usalama wa wanafunzi katika kipindi cha mvua za El Niño.
Akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba yaliyofanyika shuleni hapo, Mkurugenzi wa Shule za Hope Justa Dede, amesema wamejipanga kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama muda wote wanapokuwa shuleni.
Amesema, miundombinu ya shule hiyo iko katika hali nzuri, huku ikiwa na magari ya kutosha kwa ajili ya usafiri wa wanafunzi wa kutwa, hivyo hakuna sababu ya wazazi kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa watoto wao wakati wa mvua hizo.
“Tumekuwa tumejipanga kuhakikisha muda wote wanafunzi wanapokuwa shuleni watakuwa salama. miundombinu yetu iko vizuri na usafiri wa magari kwa wanafunzi wa kutwa upo wa kutosha hata katika kipindi cha mvua za El Niño,” amesema Dede.
Aidha, Mkuu wa Shule za Hope Daniel Rafael amewaomba wazazi kupeleka watoto wao katika shule hiyo, akisema kuwapeleka watoto shule zilizo mbali kunaweza kuwaongezea usumbufu wa usafiri na kuwafanya wazazi washindwe kufuatilia kwa ukaribu maendeleo yao ya kitaaluma.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Godlisen Masawe kutoka Exim Bank, amewataka wazazi kufuatilia kwa karibu mienendo ya watoto wao, hasa wanapokuwa nyumbani, pamoja na matumizi yao ya simu.
Amesema, baadhi ya wanafunzi hutumia simu vibaya kwa kujikita katika mitandao ya kijamii, jambo ambalo linaweza kuathiri maadili na mwenendo wao.
Masawe amewasisitiza wazazi kuwa na ushirikiano wa karibu na watoto wao, pamoja na kufuatilia matumizi ya teknolojia ili kuhakikisha wanaitumia kwa manufaa ya elimu na maendeleo yao.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkurugenzi wa Shule za Hope Justa Dede akizungumza.
kuu wa Shule za Hope Daniel Rafael akizungumza.
Mgeni Rasmi kitoka Exim Bank Godlisen Masawe.