Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025–2030, vitongoji vyote nchini vitapatiwa umeme wa REA, na kwamba katika Kijiji cha Kituli, vitongoji vinne vitasambaziwa huduma hiyo.
Azza amebainisha hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kituli wilayani Shinyanga, kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu.
TAZAMA VIDEO👇👇
Amesema ndani ya miezi tisa ya utawala wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika usambazaji wa umeme wa REA, Kijiji cha Kituli kimepata vitongoji vinne, ambavyo ni Kisumvani chenye kaya 197; Mwasami kaya 108, Sengerema kaya 95, na Ipanda kaya 86, na hivyo kufanya jumla ya Kaya 486 ambazo zitapata huduma hiyo.
“Hii ndiyo kazi ambayo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameanza nayo kwenye suala la umeme kwa wananchi wa Kituli,” amesema Azza.
Aidha, amezungumzia changamoto ya maji kwa wananchi wa Kituli, akisema kuwa tatizo hilo ni ajenda ya Jimbo la Itwangi na amekuwa akilisemea Bungeni.
Amesema, mashine ililetwa katika Shule ya Sekondari Kituli kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji, na kwamba hatua inayofuata ni kuweka pampu na miundombinu mingine, ili maji yaanze kutumika.
Amesema, pia vitawekwa vituo viwili vya kuchotea maji kwa wananchi ili wanufaike wakati wakisubiri huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria.
Kwa upande wake, Meneja wa Maji Kanda ya Tinde, Mhandisi Joshua Matinde, amesema kwa upande wa Kituli wana mpango wa muda mfupi na wa muda mrefu.
Amesema mpango wa muda mfupi ni kuchimba kisima cha maji, huku mpango wa muda mrefu ukiwa ni kusambaza maji kutoka Ziwa Victoria.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kituli.

Diwani wa Tinde Jafari Kanolo akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464