FIKRA MPYA YAWANOA MACHAMPION WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Shirika la Fikra Mpya limeendesha mafunzo kwa machampion wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambao watahusika kuwezesha upatikanaji wa haki kwa manusura wa vitendo hivyo.
TAZAMA VIDEO👇👇
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya, Leah Josiah, amesema shirika hilo linatekeleza mradi wa kuwezesha upatikanaji wa haki kwa manusura wa ukatili wa kijinsia (Justice For Survivors J4S) unaotekelezwa katika kata nne.
Amezitaja kata hizo kuwa ni Ndembezi na Ngokolo zilizopo Manispaa ya Shinyanga, pamoja na Mwataga na Igaga zilizopo Wilaya ya Kishapu.
“Mafunzo haya yatawasaidia machampion katika kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii, pamoja na kwenda kuzalisha machampion wengine katika maeneo yao na kuleta mabadiliko,” amesema Leah.
Mmoja wa machampion hao Mhoja Ibengwe kutoka Ndembezi, amesema anashukuru kupatiwa mafunzo hayo, ambayo ni msaada mkubwa kwake katika kupambana na vitendo vya ukatili.
Amesema, atakuwa balozi mzuri kwa vijana wenzake kwa kuwahamasisha kupinga vitendo vya ukatili katika jamii.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Jonh Shija kutoka Shirika la Huduma za Msaada wa Kisheria (PACESH), Mkoa wa Shinyanga, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo machampion, kuhusu huduma wanazoweza kuzitoa kwa jamii, katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, pamoja na kusaidia manusura wa ukatili kupata haki zao.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah, akizungumza.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah, akizungumza.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah, akizungumza.
Mkurugenzi wa Shirika la PACESH John Shija akitoa mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464