MIRADI 45 YENYE THAMANI YA BILIONI 18 KUMULIKWA NA MWENGE WA UHURU SHINYANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amesema Mwenge wa uhuru ambao umeanza kukimbizwa katika mkoa huo, utamulika jumla ya miradi 45 yenye thamani ya sh. bilioni 18.
TAZAMA VIDEO👇👇
Amebainisha hayo leo Agosti 18, 2026, wakati akipokea Mwenge huo kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, ambao utakimbizwa umbali wa kilomita 739.
Amesema, Mwenge huo utaweka mawe ya msingi, kufungua, kuzindua na kutembelea jumla ya miradi 45, ambapo miradi 13 itawekewa mawe ya msingi, miradi 17 itazinduliwa, miradi minne itafunguliwa, na miradi 11 itatembelewa na kukaguliwa, sambamba na shughuli za upandaji miti.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464