📌Aipongeza Wizara Ya Maliasili na Utalii kutangaza fursa za utalii nje ya nchi

📌Jaji Mruma naye atembelea Banda la Maliasili kujionea wanyamapori hai Nane Nane

Na Neema Chalila Mbuja, Dodoma

BALOZI wa Tanzania nchini Italia na Mwakilishi Mkazi  wa Shirika la Chakula na Kilimo la  Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP),  Mhe. Mbarouk  Nassoro Mbarouk leo Agosti 04, 2026,  ametembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii  na kusema kuwa nchi ya Italia ina nafasi kubwa ya kuleta watalii wengi nchini.

Mhe. Balozi Mbarouk amesema Tanzania inafanya vizuri kwenye kutangaza utalii na vivutio vyake  na kuipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayoifanya.

Katika hatua nyingine Wizara ya Maliasili na Utalii  imepokea ugeni wa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Rajab Mruma ambaye ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kubuni mbinu za kutafuta utatuzi wa  changamoto za wanyamapori hai kuingia kwenye makazi ya wananchi kwa kujenga  uzio ili kuzuia uharibifu unaoweza kutokea.

Aidha, Mhe Jaji Mruma ametembelea bustani ya wanyamapori  hai iliyoko kwenye Maonesho ya Nane  Nane yanayoendelea Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kutangaza utalii wa ndani kwa wananchi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464