Wakala wa Vipimo (WMA) umeshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnara wa Mashujaa, Mtumba, jijini Dodoma, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika leo Julai 25,2026 yamewakutanisha viongozi wa Serikali, taasisi mbalimbali za umma na binafsi, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi kwa lengo la kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliojitolea kwa ajili ya uhuru, amani na maendeleo ya Taifa.
Wakala wa Vipimo (WMA) uliwakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Alban M. Kihulla, ambaye ameshiriki pamoja na viongozi wengine wa taasisi za umma katika kuadhimisha siku hiyo muhimu ya kitaifa.
Aidha, baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dodoma wameshiriki katika maadhimisho hayo, wakionesha mshikamano na pia dhamira ya taasisi ya kuendelea kuenzi maadhimisho hayo unaakisi dhamira ya taasisi ya kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uwazi na uadilifu katika kuhakikisha usahihi wa vipimo kwenye biashara, kulinda maslahi ya walaji na wafanyabiashara, pamoja na kuchangia maendeleo ya uchuru, amani na maendeleo ya nchi, huku ikiwakumbuka mashujaa wa Taifa na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kujenga uzalendo, uwajibikaji na maendeleo endelevu.
Ushiriki wa WMA katika maadhimisho hayo unaakisi dhamira ya taasisi ya kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi, uwazi na uadilifu katika kuhakikisha usahihi wa vipimo kwenye biashara, kulinda maslahi ya walaji na wafanyabiashara, pamoja na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa.
WMA inaungana na Watanzania wote katika kuwaenzi mashujaa wa Taifa waliotoa mchango mkubwa kwa ajili ya uhuru, amani na maendeleo ya nchi, huku ikiendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji na utumishi wa umma.



