
Kauli hiyo ilitolewa katika Makao Makuu ya chuo hicho kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam na Mkuu wa chuo, Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge, wakati wa mahafali ya Kozi ya 14 yaliyowahusisha maofisa waandamizi kutoka taasisi mbalimbali za serikali, wakala, na mataifa 16 rafiki kama vile Zambia, Ethiopia, Namibia, Kenya, Bangladesh na Misri.
Balozi Ibuge alibainisha kuwa washiriki wote wa ngazi ya Stashahada na Shahada ya Uzamili katika mafunzo hayo ya miezi 11 walifaulu vizuri kozi zao za kimkakati na ulinzi kwa kina, akisema mafanikio hayo yanatokana na usimamizi mzuri wa viongozi wakuu wa nchi.
Alitoa shukrani za pekee kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi kwa ushirikiano wao mkubwa na uongozi thabiti kwa ustawi wa chuo hicho.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464