Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakisaini mkataba wa awamu ya pili wa udhamini kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027 mjini Shinyanga. 
Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakionesha jezi rasmi ya klabu baada ya kusaini mkataba wa awamu ya pili wa udhamini kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/2027 mjini Shinyanga.
Na Marco Maduhu - Shinyanga
TIMU ya soka ya Dodoma Jiji, imeingia mkataba kwa awamu nyingine wa udhamini na kampuni ya Jambo Group, kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027.
Mkataba huo wa mwaka mmoja umesainiwa leo Julai 23, 2026, katika ofisi kuu za kampuni hiyo zilizopo mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa utiaji saini Mkataba huo, Mkuu wa Ubunifu wa Mikakati na Chapa, ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group Nickson George, amesema wameamua kurefusha ushirikiano wao na Dodoma Jiji baada ya kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.
"Tumeingia mkataba huu kwa mara nyingine tena na Dodoma Jiji, ili kuendelea kuwaunga mkono katika msimu mpya wa ligi kuu. lengo letu ni kuona klabu hii inafikia malengo yake," amesema George.
Naye Mtendaji Mkuu wa Dodoma Jiji, Albert Kasoga, ameishukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kuwaamini na kuwekeza kwenye sekta ya michezo nchini, huku akiahidi kuwa timu hiyo itafanya vizuri zaidi msimu ujao wa ligi kuu.
"Tunamshukuru sana mdhamini wetu Jambo Group kwa kuendelea kuwa nasi. Tunaahidi kupambana na kufanya vizuri zaidi katika msimu huu mpya," amesema Kasoga.
Kwa upande wake, Afisa Habari na Msemaji wa Dodoma Jiji Moses Mpunga, amesema kuwa udhamini huo umekuwa nguzo muhimu katika uendeshaji wa timu na utasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha shughuli za klabu hiyo.
Mkuu wa Ubunifu wa Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George akionesha mkataba baada ya kusaini makubaliano ya awamu ya pili ya udhamini kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027 mjini Shinyanga.
Picha na Elizabeth Cosmas na Marco Maduhu
Mkuu wa Ubunifu wa Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George (kushoto), akibadilishana nyaraka za mkataba na Mtendaji Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Albert Kasoga, baada ya kusaini makubaliano ya awamu ya pili ya udhamini kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027 mjini Shinyanga.
Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakionesha jezi rasmi ya klabu baada ya kusaini mkataba wa awamu ya pili wa udhamini kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/2027 mjini Shinyanga.
Mkuu wa Ubunifu wa Mikakati na Chapa wa Jambo Group na Meneja Mkuu wa Jambo Media Group Nickson George akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba wa awamu ya pili wa udhamini kati ya Jambo Group na Dodoma Jiji FC mjini Shinyanga.
Mtendaji Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Albert Kasoga, akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa awamu ya pili wa udhamini kati ya Jambo Group na Dodoma Jiji FC mjini Shinyanga.

Msemaji wa Dodoma Jiji FC, Moses Mpunga, akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba wa awamu ya pili wa udhamini kati ya Jambo Group na Dodoma Jiji FC mjini Shinyanga.
Na Elizabeth Cosmas - Malunde 1 blog Shinyanga
Kampuni ya Jambo Group imeongeza mwaka mwingine wa udhamini kwa klabu ya Dodoma Jiji FC baada ya kusaini mkataba wa awamu ya pili wa ushirikiano kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/2027.
Mkataba huo wa mwaka mmoja umesainiwa leo Julai 23, 2026, katika ofisi kuu za Jambo Group zilizopo mkoani Shinyanga, ukihudhuriwa na viongozi wa kampuni hiyo pamoja na uongozi wa klabu ya Dodoma Jiji.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini, Mkuu wa Ubunifu wa Mikakati na Chapa wa Jambo Group ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Jambo Media Group, Nickson George, amesema kampuni hiyo imeamua kurefusha ushirikiano wake na Dodoma Jiji kutokana na kuridhishwa na mafanikio na mwenendo wa timu hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
"Tumeingia mkataba huu kwa mara nyingine tena na Dodoma Jiji ili kuendelea kuwaunga mkono katika msimu mpya wa Ligi Kuu. Lengo letu ni kuona klabu hii inafikia malengo yake," amesema George.
Ameongeza kuwa mwaka jana Jambo Group ilianza rasmi ushirikiano na timu hiyo kwa kutumia kaulimbiu ya "Zege la Zabibu", huku mwaka huu wakija na kaulimbiu mpya ya "Zabibu Zimerefushwa" kuashiria kuongezwa kwa mkataba wa ushirikiano.
"Maana halisi ya kaulimbiu yetu ya 'Zabibu Zimerefushwa' ni kwamba sisi Jambo Group tumerefusha mkataba wetu na timu ya Dodoma. Hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri uliokuwepo mwaka jana na dhamira yetu ni kuendelea kutoa mchango katika sekta ya michezo pamoja na kuja na mikakati bora zaidi katika msimu unaokuja," amesema George.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Dodoma Jiji FC, Albert Kasoga, ameishukuru Jambo Group kwa kuendelea kuiamini klabu hiyo na kuwekeza katika maendeleo ya michezo nchini.
"Tunamshukuru sana mdhamini wetu Jambo Group kwa kuendelea kuwa nasi. Tunaahidi kupambana na kufanya vizuri zaidi katika msimu huu mpya," amesema Kasoga.
Naye Afisa Habari na Msemaji wa Dodoma Jiji FC, Moses Mpunga, amesema ushirikiano huo umekuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya timu na umechangia mafanikio mbalimbali ndani na nje ya uwanja.
"Msimu uliopita ulikuwa msimu mzuri kwetu tukiwa chini ya udhamini wa Jambo Group. Kupitia ushirikiano huo, timu iliweza kufanya vizuri katika vipindi tofauti, na yote haya ni matokeo ya ushirikiano wetu. Kwa hiyo, kuongezwa kwa mkataba huu wa awamu ya pili kutatusaidia kufanya vizuri zaidi katika msimu unaofuata," amesema Mpunga.
Amesema mbali na kusaidia shughuli za michezo, Jambo Group imeendelea kuisapoti Dodoma Jiji katika maeneo mengine ya kijamii ikiwemo afya na usafi wa mazingira.
"Kupitia ushirikiano huu, Jambo Group imeweza kutusapoti pia katika sekta nyingine kama afya pamoja na usafi wa mazingira, kwa kutupatia vifaa na T-shirt. Kwa hiyo, kupitia ushirikiano wetu huu, tunaamini tunaweza kufanya vizuri zaidi," amesema.
Aidha, Mpunga amebainisha kuwa klabu hiyo inajiandaa kuandaa mechi maalumu kubwa itakayofanyika mkoani Shinyanga chini ya udhamini wa Jambo Group, ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza na kuwazawadia mashabiki wa soka wa mkoa huo.




























