` JAMBO YAIDHAMINI GEITA GOLD MSIMU WA LIGI KUU TANZANIA BARA

WANDAMAN HOTEL

JAMBO YAIDHAMINI GEITA GOLD MSIMU WA LIGI KUU TANZANIA BARA



Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Klabu ya soka ya Geita Gold imesaini mkataba wa udhamini na kampuni ya Jambo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) wa mwaka 2026/2027.

TAZAMA VIDEO👇👇


Mkataba huo wa mwaka mmoja umesainiwa leo Julai 28, 2026 mjini hapa, ukiwa na lengo la kuiongezea nguvu klabu hiyo katika kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano hiyo.
Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo, Mkuu wa Ubunifu wa Mikakati na Chapa, ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Jambo Media Nickson George, amesema wameamua kuingia makubaliano hayo ili kupanua wigo wa uwekezaji wao kwenye soka la ndani.

"Katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, tumeamua kuongeza ushirika na timu ya Geita Gold, kwa kuidhamini kwa msimu mzima wa 2026/2027, na udhamini huu utadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja," amesema George.
Naye Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Geita Gold, Gilbert Mwaisunga, ametoa shukrani zake kwa kampuni hiyo kwa kujiunga na familia ya Geita Gold, huku akisisitiza kuwa klabu za mikoani zinahitaji kuungwa mkono ili kuleta ushindani wa kweli kwenye ligi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Geita Gold Zengo pole, amesema wanayofuraha kubwa kwa kukutana na jambo na kuanzisha ushirika, na timu hiyo imekuwa familia moja na Shinyanga.


TAZAMA PICHA👇👇

Mkuu wa Ubunifu wa Mikakati na Chapa, ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Jambo Media Nickson George (kulia) akiwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Geita Gold, Gilbert Mwaisunga, wakisaini mkataba wa udhamini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464