
Akizungumza katika kikao hicho, Bandora amesema kuwa maendeleo ya Kata ya Chemchem yanategemea ushirikiano wa viongozi, wataalamu na wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na mipango madhubuti itakayoongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Aidha, amesisitiza kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kuishi katika mazingira salama na yenye utulivu.
Katika hatua nyingine, Bandora amewataka wenyeviti wa mitaa kufanya vikao vya mara kwa mara na wananchi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto pamoja na kero zinazowakabili, huku akiwahimiza wataalamu wa kata kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi.
Amesema kuwa uwajibikaji wa kila mmoja utasaidia kuendana na kasi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kaulimbiu: Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464