
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika kukuza ushirikiano na Urusi, Tanzania itaendelea na mipango yake ya maendeleo pamoja na washirika wengine wa kimataifa kwani haijawekewa vikwazo vyovyote.
"Nataka nikuhakikishie kwamba Tanzania hatupo kabisa kwenye Sanctions (vikwazo) na tunajipanga kufanya maendeleo yetu," amesema Rais Samia.
Rais ameeleza hayo Juni 5, 2026 wakati akijibu swali la mwendesha mada katika Jukwaa la Kimataifa la Kiuchumi la St. Petersburg (SPIEF) nchini Urusi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464