` MCHUNGAJI HANANJA AONYA MATUMIZI YA HOVYO YA MITANDAO

WANDAMAN HOTEL

MCHUNGAJI HANANJA AONYA MATUMIZI YA HOVYO YA MITANDAO



Mchungaji Richard Hananja amewataka vijana kutafakari kwa kina kabla ya kushiriki katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa tofauti za mitazamo zinapaswa kuwa chachu ya mazungumzo na maelewano badala ya kusababisha migawanyiko katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Hananja amesema matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii yanaweza kuchochea chuki, matusi na vurugu, hali inayoweza kuathiri mshikamano wa kitaifa.

Amehimiza vijana kutumia majukwaa ya kidijitali kwa uwajibikaji, kuheshimu maoni ya wengine na kuendeleza maadili yanayojenga umoja, amani na maendeleo ya jamii.

Hananja amesisitiza kuwa vijana wana nafasi muhimu katika kulinda amani ya taifa na kwamba ushiriki wao katika mijadala ya kijamii na kisiasa unapaswa kuongozwa na busara, heshima na uzalendo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464