` DC MTATIRO AENDELEA NA KLINIKI YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

WANDAMAN HOTEL

DC MTATIRO AENDELEA NA KLINIKI YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 

DC MTATIRO AENDELEA NA KLINIKI YA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, ameendelea na kliniki ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, safari amekutana na wakazi wa Tarafa ya Nindo.

Akizungumza leo Juni 13, 2026 wakati wa mkutano huo, Mtatiro amesema jukumu la viongozi ni kusikiliza changamoto za wananchi na kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma na kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Amesisitiza kuwa, katika kushughulikia malalamiko hayo, haki itazingatiwa kwa kila upande kwa mujibu wa sheria.

“Mimi kwenye masuala ya haki siwezi kuteteleka katika kliniki hii mwenye haki atapata haki yake” amesema Mtatiro.
Pia ameagiza timu inayoshughulikia utatuzi wa kero hizo kuhakikisha inazimaliza ndani ya siku 14.

Katika mkutano huo, wananchi wa Tarafa ya Nindo waliwasilisha kero mbalimbali zikiwamo migogoro ya ardhi na mipaka, ubovu wa miundombinu ya barabara, changamoto za huduma ya umeme, maji, afya, pamoja na masuala ya mirathi.

MAELEZO YA PICHA👇👇

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464