` SERIKALI KUENDESHA CHANJO YA MATONE YA POLIO AWAMU YA PILI

WANDAMAN HOTEL

SERIKALI KUENDESHA CHANJO YA MATONE YA POLIO AWAMU YA PILI


Mratibu wa chanjo manispaa ya Shinyanga Ramadhani Maneno  akizungumza

Mwakilishi kutoka ofisi ya waziri mkuu TAMISEMA idara ya afya Linda Chatila

Na Eunice Kanumba –Shinyanga

Serikali kupitia wizara ya afya inatarajia kuendesha zoezi la utoaji wa chanjo ya matone ya polio kuanzia tarehe 7 hadi 10 may 2026  kwa  watoto chini ya miaka kumi ikiwa ni awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza kutolewa kwa watoto wa umri huo mwezi march 2026.

Katika kujenga uelewa wa pamoja  juu ya chanjo hiyo  ili kuwafikia walengwa  serikali  leo tarehe 4 maya 2026 imeendesha  mafunzo kwa wadau wenye ushawishi kutoka katika jamii, ili zoezi hilo la chanjo  kwa awamu ya pili liweze kutekelezeka kwa ufasaha.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada juu ya ugonjwa  wa polio  na chanjo hiyo mratibu wa chanjo manispaa ya Shinyanga Ramadhani Maneno   amesema  lengo la mafunzo ni kujengeana uelewa wa pamoja juu ya nini kinachokwenda kufanywa na serikali katika zoezi la kitaifa linalojumuisha mikoa ya Shinyanga,Geita Mara Singida Simiyu Kagera na Tabora.

Amesema kwa upande wa manispaa ya Shinyanga Jumla ya watoto 71,966 wanaoanzia umri wa miaka kumi kushuka chini wanatarajiwa kupatiwa chanjo kwa amu ya pili ili kuwajengea kinga Zaidi juu ya ugonjwa huo hatari  unaopelekea mtoto kupooza na  kupata ulemavu wa ghafla.

Maneno ameanisha kuwa  katika kutekeleza jukumu hilo kwa weledi  manispaa ya Shinyanga tayari imeandaa timu 91 zitakazohudumia jamii ambapo timu 83 zitatembea nyumba kwa nyumba kutoa huduma za chanjo hiyo huku timu 8 zikipita katika maeneo maalum kama vile katika  masoko na maeneo ili kuhakikisha hakuna mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi anakosa chanjo hiyo kwa ustawi wa jamii imara.

Naye muwakilishi kutoka ofisi ya waziri mkuu TAMISEMA idara ya afya Linda Chatila amesema chanjo hiyo sio jambo jipya ilikuwa ikitolewa hata siku za nyuma lakini kwa sasa inatolewa kwa kampeni maalum kufuatia kugundulika vimelea vya ugonjwa huo katika maji taka jijini Mwanza hali iyopelekea serikali kuchukua hatua za maksudi ilikuinusru jamii na ugoonjwa huo.

“Polio haina tiba, lakini inazuilika kwa chanjo. Ni muhimu wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hii kwa wakati,” amesema Chatila

Amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni salama kwa watoto wote walio chini ya miaka 10, na kuonya kuwa mtoto atakayekosa chanjo atakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo huku akiwasihi wazazi kuachana na uvumi potofu juu ya chanjo hiyo kwamba ina madahra kwa watoto na kuanisha kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la afya duniani (WHO) pamoja na wizara ya afya na masuala ya vifaa ya tiba (TMDA).

Nao  baadhi ya wadau walioudhuria mafunzo akiwemo John Kadama kamanda mkuu wa sungusungu mkoa wa Shinyanga ambaye amesema kuwa  ameipongeza serikali kwa uamuzi huo wa kuwanusuru watoto dhidi ya ugonjwa huo na kwamba jeshi la sungusungu litatoa ushrikiano ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika ipasavyo.

Naye menyekiti wa baraza ushauri la wazee manispaa ya Shinyanga Stephano Tano amewaasa wazazi na walezi kuhakikisha watoto walio chini ya umri wa miaka kumi wanapatiwa chanjo hiyo ili kuzuia lemavu na vifo kwa watoto.

MWISHO

PICHA ZA WASHIRKI /WADAU HAPA CHINI  

 









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464