` DIWANI TANDIKO APELEKA KICHEKO CHA EID AL- ADHA KWA WANANCHI WA MAGANZO

WANDAMAN HOTEL

DIWANI TANDIKO APELEKA KICHEKO CHA EID AL- ADHA KWA WANANCHI WA MAGANZO

Kishapu


Diwani wa Kata ya Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Hamza Tandiko, amesherehekea Sikukuu ya Eid Al-Adha kwa kuandaa karamu ya pamoja na wananchi wa Kata hiyo.


Karamu hiyo iliyofanyika Mei 27, 2026, iliwakutanisha wananchi mbalimbali waliohudhuria nyumbani kwa Diwani huyo kushiriki chakula, vinywaji na kuendeleza mshikamano wa kijamii katika siku hiyo muhimu kwa Waislamu duniani kote.



Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Tandiko amesema lengo la kuandaa karamu hiyo ni kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na mafanikio anayoendelea kumpatia yeye pamoja na familia yake, sambamba na kuimarisha upendo na umoja miongoni mwa wananchi wa Maganzo.



“Ni muhimu kushirikiana na jamii katika nyakati kama hizi za sikukuu ili kuendeleza upendo, mshikamano na kuwajali wenye uhitaji, lakini haya yote yatatimia endapo tu tutahakikisha kila mmoja wetu ni balozi mzuri na mlinzi wa amani ya jamii na taifa letu kwa ujumla” ameongeza Mhe. Tandiko.





Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wamempongeza diwani huyo kwa moyo wake wa ukarimu na kujitoa kwa jamii, wakisema ni kiongozi mwenye huruma na anayependa kuwaweka watu pamoja.



“Amekuwa mtu wa mfano katika jamii hata kabla hajwa Diwani ana moyo wa upendo, huruma na kujali wananchi wake bila ubaguzi. Mungu azidi kumbariki kwa kututhamini na kutujali sisi wananchi,” wamesema baadhi ya wananchi hao.



Sikukuu ya Eid Al-Adha, maarufu pia kama sikukuu ya “Kuchinja”, huadhimishwa na Waislamu duniani kote ikiwa ni kumbukumbu ya utiifu wa Nabii Ibrahim (A.S) kwa Mwenyezi Mungu. Sikukuu hiyo hufundisha jamii umuhimu wa upendo, kusaidiana, kusameheana na kuwajali wenye uhitaji ili kuendeleza amani na mshikamano katika jamii.






































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464