` UFUNGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA ROYAL MKOMBOZI KWA WATANZANIA

WANDAMAN HOTEL

UFUNGUZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA ROYAL MKOMBOZI KWA WATANZANIA



Na Edwin Soko, Mwanza.

Kesho Mei 10, 2026 rasmi Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Royal itafunguliwa na kutoa nafasi ya watanzania hususani wakazi wa Kanda ya Ziwa kunufaika na huduma bora na za kisasa za afya.

Mgeni Rasmi anataraji kuwa Askofu Mkuu ni Rev Dr . Barnabas W. Mtokambali

Ujio wa Hospital hiyo ya Rufaa ya Kanda unataraji kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa ambao walisubiri kwa muda mrefu na kesho watashiriki kwenye ufunguzi huo kwa shauku kubwa .

Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Royal Dkt. Lusako Mwaikasu alisema kuwa, Shughuli zote za maandalizi ya ufunguzi hapo kesho zimekamilika na wageni mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya Nchi wamewasili tayari Jijini Mwanza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Glory Simon amewahakikishia

watanzania kuwa, Hospitali ya Rufaa ya Royal itafanya kazi kwa ufanisi mkubwa hivyo watanzania wategemee kunufaika na huduma bora za afya.

Naye Bwana Richard Nickson wa Ghana Jijini Mwanza amesema kuwa, wana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla wamepokea kwa mikono miwili taarifa za ufunguzi wa Hospitali hiyo ya Rufaa kwani hiyo ni taarifa njema inayokwenda kuleta tija kwenye sekta ya afya.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Royal ipo mtaa wa Ghana Jijini Mwanza, Kanda ya Ziwa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464