Benki ya TADB Yapongezwa kutoa mikopo Sekta ya Mifugo
Edwin Soko
Busanda, Shinyanga
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Agnes Meena, ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa mchango wake mkubwa katika kutoa mitaji inayowezesha maendeleo ya sekta ya mifugo nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Mifugo Kanda ya Ziwa 2026, Bi. Meena alisema TADB imekuwa chachu ya kuongeza tija, uzalishaji na kukuza ufugaji wa kibiashara, huku akiiomba benki hiyo na wadau wengine kuendelea kutatua changamoto za wafugaji kwa wakati.
Kwa upande wake,
Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TADB, Andrew Kimbelwa, amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na wafugaji na wadau wa sekta ya mifugo ili kuhakikisha wanapata mitaji na huduma za kifedha zinazowawezesha kuongeza uzalishaji.
Hadi sasa, TADB imetoa mitaji ya zaidi ya TZS Bilioni 119 kwa maendeleo ya sekta ya mifugo nchini, ambapo TZS Bilioni 25 zimetolewa katika Kanda ya Ziwa pekee, zikinufaisha zaidi ya Watanzania 60,000.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464


