` CHEREHANI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA 29 YA WIKI YA MAZIWA KITAIFA IRINGA

WANDAMAN HOTEL

CHEREHANI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA 29 YA WIKI YA MAZIWA KITAIFA IRINGA

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Cherehani akinywa maziwa kwenye Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa Mei 31, 2026 katika Viwanja vya Mwembe Togwa, mjini Iringa.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Cherehani, ameshiriki ufunguzi wa Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yaliyofanyika leo Mei 31, 2026 katika Viwanja vya Mwembe Togwa, mjini Iringa.

Mgeni rasmi katika ufunguzi huo alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Mb), ambaye amefungua rasmi maadhimisho hayo yanayolenga kuhamasisha maendeleo ya sekta ya maziwa nchini kupitia uzalishaji, uchakataji na biashara ya maziwa yenye tija kwa wafugaji na taifa kwa ujumla.

Mhe. Cherehani ameshiriki hafla hiyo akiwa pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deodatus Mwanyika, ambao wamepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonesho na kujionea shughuli zinazofanywa na wadau wa sekta ya maziwa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mwaka 2026 yanafanyika mkoani Iringa pamoja na maeneo mengine ya nchi yakiongozwa na kaulimbiu isemayo, "Rasimisha Biashara ya Maziwa, Okoa Maisha ya Walaji, Ongeza Kipato, Changia Uchumi."

Kaulimbiu hiyo inalenga kuhamasisha urasimishaji wa biashara ya maziwa ili kuhakikisha usalama wa walaji, kuongeza kipato kwa wafugaji na wafanyabiashara wa maziwa, pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia sekta ya mifugo.

Maadhimisho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maziwa wakiwemo wafugaji, wasindikaji wa maziwa, wafanyabiashara, taasisi za serikali na binafsi pamoja na washirika wa maendeleo kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuonesha teknolojia za kisasa na kujadili fursa zilizopo katika kuendeleza sekta ya maziwa nchini.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Cherehani akiwasalimia washiriki wa Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa Mei 31, 2026 katika Viwanja vya Mwembe Togwa, mjini Iringa. 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464