
Maonesho hayo
yanayodhaminiwa na benki ya CRDB yamelenga kufungua fursa zaidi kwa wafugaji na
pia kutatua changamoto za kufuga Wakati huu ambao wafugaji wengi wanakabiliwa
na upungufu wa utaalamu wa kisasa jambo linalosababisha mifugo kufa na kupata
hasara.

Muandaaji wa maoneshio hayo Bw. Charles Nduku kutoka kampuni ya Farm Flex group amesema Maonesho haya yanatarajiwa kuleta mapinduzi katika sekta ya ufugaji na kuboresha uchumi wa wakazi wa kanda hiyo yatachagizwa na mashindano ya michezo mbalimbali ukiwemo mchezo maarufu kanda ya ziwa wa mbio za baiskeli.
Aidha amesema katika maonesho hayo wataalikwa wataalamu
mbalimbali watakaotoa elimu ya ufugaji wa kibisashara ili wafugaji wajifunze
mbinu za kufuga kisasa na kukidhi soko la kimataifa.
Akionesha mfano kuwa mfugaji anaweza kufuga ng’ombe wengi kiholela
bila kupata mafanikio kwa kuuza kwa bei ndogo ng’ombe mmoja kwa shilingi laki mbili
mpaka tatu lakini kwenye manesho hayo akajifunza kufuga mifugo wachache kitaalamu
na akauza ng’ombe mmoja kwa shilingi milioni moja hadi mbili na kupata faida ya
kutosha.
Hata hivyo ameenda mbali zaidi akiangazia ufugaji wa mataifa
mengine na masoko ya kimataifa kuwa kwa kawaida walaji wa maeneo hayo wananunua
kitoweo cha nyama au bidhaa zingine zitojanazo na mifugo kwa kufuata historia
ya Wanyama hao.

Jumaane Wambura Wagana ni meneja wa CRDB kanda ya magharibi amesema Benki hiyo imedhamini maonesho hayo na kukabidhi hundi ya shilingi Milioni 20 kama wadhamini wakuu wa maonesho hayo huku akiwashauri wafugaji kukata bima ya mifgugo ili kutatua changamoto ya kupata hasara.
Aidha Bw. Wagana Wambura amesema Benki ya CRDB imeingia
mkataba na chama cha wafugaji nchini kuwakopesha wakulima mikopo yenye riba
nafuu ili kuwainua kiuchumi wafugaji huku akiwahimiza wafugaji kuchangamkia
fursa hiyo.
Aidha wagana amesema katika kipindi chote cha maonesho hayo Benki
ya CRDB itakuwa pale muda wote kuhakikisha kwamba inawafungulia fursa ya kupata
mtaji wafugaji wa aina zote na wanaofuga ng’ombe, mbuzi, kuku na Wanyama wengine
lengo likiwa ni kuhakikisha kila anayehusika na kujongea kutafuta fursa hiyo anafikiwa
kikamilifu nakupatiwa kile anachohitaji.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464