

Na Kareny Masasy,
Kahama
KATIBU wa Nec,Siasa Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Rabia Hamad ,amesema kuna mkakati wa kuweka machinga Complex kwenye kila wilaya ili machinga wote wawe sehemu moja nakuweza kutambulika.
Hamad amesema tarehe 26/03/2026 kwenye kikao kazi wilayani Kahama kilichowakutanisha makundi ya wajasiliamali, Watu wenye Walemavu,Wachimbaji Wadogo na Wawezeshaji wanawake kiuchumi huku akisisiiza kukopa kwenye Halmashauri na Benki ambako kuna fedha ziko huko.
Hamad alisema wajasiriamali waendelee kukaa kwenye vikundi nakupata mikopo isiyo na riba kwenye Halmashauri na ile ambayo Rais Samia Suluhu aliitoa kwenye benk ya NMB kwa mashariti nafuu na lazima uwe na kitambulisho cha mjasiliamali.
“Viongozi mnapoona kimpya muhoji kwanini hiki hakijatekelezwa au kimefikia wapi ili ngazi ya juu iweze kulifanyia kazi”amesema Hamad.
Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalum Slyilivia Lusumo alisema wafanyabiashara wote wadogo wanatakiwa kutambulika kwa mauzo kwa mwaka yasizidi Milioni Nne huku wakitoa changamoto ya fursa za mikopo haziwafikii.
“Serikali imetoa shilingi bilioni 200 na zimewekwa katika mgawanyo mpaka sasa zimetolewa bilioni 12 na nchi nzima na mkoa wa Shinyanga zimetolewa shilingi Milioni 255 kwa wafanyabiashara 124”amesema Lusumo.
Lusumo alisema wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga waliosajiliwa ni 1556 na waliosajiliwa ni wafanyabiashara ni 750 na utaratibu wa kupata mkopo nilazima uwe umesajiliwa kwenye mfumo na vigezo wawe na utambulisha wa mjasiliamali.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Khamis Mnubi alisema vigezo vya kupata mkopo kikundi lazima kisajiliwe na mkazi wa eneo husika nakuomba kupitia mkopo hivyo halmashauri inajitosheleza kwani mwaka huu wa fedha 2025/2026 wametenga billion 3 wametoa mikopo kwenye awamu mbili kuanzia mwezi Julai hadi Disemba shilingi bilioni 1.1 katika vikundi 57.
Akiongea kwa niaba ya Umoja wa machinga (Shiuma) wilaya ya Kahama Barnaba Mazengo amesema Kahama inahudumia nchi nane lakini hawana eneo maalum la machinga (Machinga compelx) ambapo hakuna miundombinu mizuri.
“Wapo wanufaika wa mikopo ambao wanamitaji tayari na wale ambao wanachuuza biashara zao mitaani hawana sifa sababu hawana kizimba nakukipata ni shilingi 50,000 nakulipa ni muda wa miezi sita na hela hawana”amesema Mazengo.
Mwisho.




.jpeg)






